Friday 6 November 2015

WANASIASA, WASOMI, WANANCHI WAMMWAGIA SIFA KEMKEM DK MAGUFULI




WANASIASA na viongozimbalimbali wamemmwagiasifa Rais wa Awamu ya Tano, Dk. John Magufuli na kusema wana imani ataipeleka Tanzania katika maendeleo ya juu.

Kutokana na imani waliyo nayo, wamewataka Watanzania sasa kuungana ili kufanya kazi kwa bidii na kuliletea taifa maendeleo endelevu.

Sambambanasifahizo, wamesema kitendo cha kupokezana uongozi ni cha kujivunia na kwamba yote hiyo ni kutokana na misingi imara ya umoja wa kitaifa iliyojengwa tangu kuasisiwa kwa taifa la Tanzania.

Wakizungumza muda mfupi baada ya kuapishwa kwenye Uwanja wa Uhuru, jijini Dar es Salaam jana, viongozi hao na wanasiasa walisema wana imani na Rais Dk. Magufuli kwamba atatekeleza ahadi zake alizotoa wakati wa kampeni, hivyo wanapaswa kuwa wavumilivu na kumuunga mkono katika kufanya kazi.

NKAMIA AFUNGUKA

Mbunge wa Chemba na aliyekuwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Juma Nkamia, alisema Watanzania wanapaswa kujivunia amani na utulivu vilivyoko nchini na kuendelea kuenzi tunu hizo ambazo ni adimu kupatikana katika taifa lolote lile.

“Ukiangalia hata viongozi wa nchi za kigeni waliokuwa katika sherehe ya leo (jana) wamekuwa wakishangaa namna Tanzania tunavyopokezana uongozi bila mikwaruzano yoyote. Kwa kweli wanajifunza mambo ambayo yanafanyika hapa nchini. Kwa hiyo ni vyema Watanzania tukatambua kuwa tuna wajibu wa kufanya kazi huku tukienzi amani yetu,” alisema.

MSEKWA FURAHA TELE

Spika wa zamani wa Bunge la Tanzania, Pius Msekwa, kwa upande wake hakusita kuelezea furaha yake pale aliposema anafurahi kuona mtu aliyeshiriki kumpigania kuwa mgombea urais, ameingia madarakani na sasa ameapishwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano wa Tanzania.

“Mimi ni miongoni mwa wazee walioshiriki kumpata mgombea wetu na leo Mungu ameweka mikono juu yake na kuwa Rais. Nawaomba wananchi wasiwe na wasiwasi na Dk. Magufuli kwa sababu ni mtekelezaji wa mambo, hivyo yale aliyoyaahidi atayatekeleza bila wasiwasi,” alisema.

ANNA ABDALLA ALONGA

Mwingine aliyekuwa na furaha isiyo kifani ni Anna Abdallah, ambaye aliwahi kuwa Waziri wa Ujenzi wakati Dk. Magufuli akiwa naibu wake kuanzia mwaka 1995 hadi 2000. Dk.Magufuli amekuwa akimtaja Anna, ambaye ni mwanasiasa mkongwe mwanamke kuwa mwalimu wake wa kazi.

Alisema ana furaha kubwa kwa sababu hiyo si mara ya kwanza kwa aliyekuwa msaidizi wake kuwa kiongozi wa ngazi za juu serikalini, kwa kuwa hata alipokuwa Waziri wa Kilimo, aliyekuwa naibu wake,Frederick Sumaye, naye alikuja kuwa Waziri Mkuu.

Akizungumzia Samia Suluhu Hassan kuwa mwanamke wa kwanza kushika nafasi ya Makamu wa Rais, alisema huo ni ushindi na ukombozi kwa wanawake wote wa Tanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla.

LUKUVI AONYA

Aliyekuwa Waziri wa Ardhi,D Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Willian Lukuvi, alisema ana imani kubwa na Rais Magufuli kwa kuwa ni mchapakazi na hana mchezo na wale wanaozembea katika kazi.

“Alisema mambo mengi wakati wa kampeni na yote aliyosema ni dhahiri atatekeleza bila wasiwasi. Watanzania wanatakiwa tu kuwau na subira na kushirikiana na serikali ya Dk. Magufuli katika kutekelezaa mambo yote. Kwa wale waliokuwak wakiendekeza ufisadi wajue kwamba(mwisho wao umefika,” alisema.

SIMBACHAWENE AFICHUA

Kwa upande wake, Mbunge mteule wa Kibakwe(CCM),George Simbachawene, alisema matarajio makubwa kuwa Dk. Magufuli ataipeleka Tanzania kwenye maendeleo makubwa ya kiuchumi na kijamii kutokana na ahadi zake kwamba atahakikisha viwanda vingiy vinajengwa maeneo mbalimbalis nchini.

Alisema Dk. Magufuli ataendelezaa mambo mema ya maendeleos yaliyofanywa na mtangulizi wake, Dk. Jakaya Kikwete, ambaye alisemai ameweka misingi imara ya kuifanya Tanzania kupaa kimaendeleo.

“Hivi sasa tumepiga hatua kubwa katika upatikanaji wa nishati, sekta ambayo nilikuwa naisimamia (akiwa Waziri wa Nishati na Madini) kwani umeme umeanza kuwepo wa kutosha na utachochea maendeleo ya viwanda mbayo ni dhamira ya Rais Dk. Magufuli,” alisema.

MEMBE ANENA

Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe, amesema ni vyema Watanzania wote kukubali kuwa Dk. John Magufuli ni Rais wa awamu ya tano wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia, alisema serikali ya Dk. JohnMagufuli haitakuwa na unafiki ila itakuwa ni ya kuleta maendeleo.

“Ushindi ni ushindi tu, uwe wa kisigino, kichogoni ni ushindi hivyo tukubali ushindi wa Rais Dk.Magufuli,” alisema Membe. Aliongeza: “Rais ameshapatikana hivi sasa Watanzania tufanye kazi tuachane na siasa.”

CHIFU WANZAGI

Chifu wa kabila la wazanaki, Japhet Wanzagi, amesema Rais Dk.Magufuli ana uwezo mkubwa wa uongozi na kuwaongoza Watanzania.

Pia, amesema Dk. Magufuli ameweza kujitangaza vyema na kukitangaza Chama cha Mapinduzi (CCM) na kutangaza sera zake na kukifanya Chama kushika hatamu kama ilivyokuwa hapo awali.

Chifu Wanzagi amesema Rais Magufuli ni mtu safi na asiyekuwa na makundi, hivyo anaamini hata serikali yake ataiendesha bila ya kufuata makundi ya watu.

“Tunajua CCM ni chama kinachoendeshwa kwa makundi, lakini kuingia kwa Rais Magufuli, makundi yote yataondoka kwa kuwa mtawala si mtu wa makundi,” alisema.

Hata hivyo, alimtaka Rais Magufuli aanze kwanza na rushwa kwa kuwa ni suala lionalomgusa kila Mtanzania.

jamani, Watanzania wa hali ya chini wanaumia, hili suala la rushwa Magufuli anatakiwa kuliondoa haraka kwani ni changamoto kubwa kwa Watanzania,” alisema.

Aliwaomba watumishi wa serikali kila eneo, kufanya kazi inavyotakiwa.

WATANZANIA WAASWA

Katika hatua nyingine, Watanzania wametakiwa kuto sherehekea kupatikana kwa rais mpya, badala ,yake washiriki kikamilifu kuimarisha misingi imara iliyowekwa na waasisi wa taifa, ikiwemo kulinda uhuru na kuendeleza dhana ya kujitegemea.

Vilevile, wametakiwakuwah watulivu na kuacha ushabiki nai uzushi ili maridhiano kuhusu suala laZanzibar yaweze kufikia muafaka.

Dk. Bashiru Ally, Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaa, ambaye pia ni mchambuzi wa masuala ya siasa, alisema hayo jana, jijini Dar es Salaam, wakati akitoa maoni yake kufuatia kuapishwa kwa Rais mpya wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli.

“Waasisi wa taifa la Tanzania, Hayati Mwalimu Julius Nyerere na Abeid Amani Karume, walijenga misingi ya taifa la watu wenye uwezo wa kujitegemea, hivyo kila mwananchi anatakiwa kuendeleza kazi hiyo ya kihistoria ili kuliendeleza taifa.” alisema.

Aliwataka wananchi kutojidanganya, bali waondoe dhana ya kuletewa mabadiliko na wanasiasa kwa kuwa maendeleo ni kazi ngumu inayohitaji mapambano na ushiriki wa kila mmoja kuinua uchumi binafsi na wa taifa.

“Maendeleo kamwe hayawezi kuletwa na rais pekee, bali yanapaswa kufanywa kwa pamoja, ikiwemo ushirikiano wa jumuia mbalimbali ambazo Tanzania ni nchi mwanachama,î alisema Dk. Bashiru.

Alisisitiza kuwa pamoja na nia yake nzuri ya kuliletea taifa maendeleo, Rais Magufuli hana namna ambayo anaweza kuleta mabadiliko pasipo ushirikiano wa ndani na nje ya nchi.

Alisema si jambo zuri kwa vyama vinavyounda UKAWA kujitenga na kutohudhuria sherehe za kuapishwa kwa Rais Magufuli, kwa kuwa ni suala linaloweza kupunguza uwezo wa kupeleka nchi pale inapokusudiwa.

“Iwapo kweli wanayo mapenzi mema na nchi hii, waache zilizojitokeza ili kusukuma gurudumu la maendeleo kufikia kule kunakotarajiwa kwani maendeleo si zawadi, ni mapambano, alisema.

Alisema yapo mambo ambayo serikali ikifanya,yanaweza kuwarudisha kwenye mstari wapinzani, ikiwemo uteuzi makini wa Waziri Mkuu na baraza la mawaziri, hotuba makini na utendaji bora, kama ilivyokuwa miaka mitano iliyopita.

“Lakinihaifaiwapinzani kudekezwa kwani wanaweza kuleta shida kwa kuwa mara nyingi huwa ni wachonganishi, kwa mfano walianza kuleta harufu ya mgawanyiko wa dini, ukabila na ukanda,î alisema.

Aliwataka wananchi kutumia utashi wao na kutambua kuwa vyama vyao vinaweza kuwaburuza kwa hoja potofu na mwishowe kuwaacha kama walivyo.

“Watu waache ushabiki wa kisiasa bila kufikiri kuwa wanaweza kuleta demokrasia kwa vyama vyao vya siasa na vikajisahau, jambo ambalo ni hatari kwa taifa. Nchi bado ina umoja na mshikamano, wawe watu wanaoweza kugundua kuwa mtu fulani hana maslahi kwa maendeleo ya taifa.’’ alisema.

Alizitaka taasisi zote za serikali na binafsi kufanya kazi kwa bidii badala ya kubweteka na kuwafanya Watanzania kuwa wadadisi, bali wawe wafuatiliaji na huku wakitoa mchango kwa taifa.

Dk. Bashiru alisema Rais Magufuli anapaswa kutambua kuwa kiu ya Watanzania ni kuona viongozi wanaoishi maisha yanayofanana na wao, ambao wanachukizwa na mtindo wa maisha ya anasa kwa viongozi huku wao wakipata shida.

“Katika nchi maskini, watu wanataka mabadiliko ya maisha hususan watoto wao kumudu kupata elimu na upatikanaji wa kutosha wa dawa hospitalini,î alisema.

Akihojiwa na kituo kimoja cha televisheni baada ya Rais Magufulikuapishwa,Makongoro Nyerere, alimpongeza kwa ushindi na kuwataka Watanzania wasiopenda kuwajibika wajiandae kwa kuwa hapa kazi tu.

Mzee aliyetajwa kwa jina moja la Masalakulagwa, ambaye alifanya kazi pamoja na Hayati Mwalimu Nyerere, alishukuru kumalizika salama kwa uchaguzi na kumtaka Rais Magufuli kufanyia kazi kasoro zote ambazo zimekuwa kero kwa wananchi.

No comments:

Post a Comment