 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akisalimiana na Balozi wa Japan nchini Masaharu Yoshida
aliyefika Ikulu Jijini Dar es Salaam kwa ajili ya mazungumzo. Katika
mazungumzo hayo Balozi Yoshida amempongeza Rais Magufuli kwa kuchaguliwa
kuiongoza Tanzania katika awamu hii ya tano na pia amezungumzia miradi
mbalimbali inayofadhiliwa na Japan hapa nchini. |
 |
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe
Magufuli akipokea Kalenda kutoka kwa Balozi wa Japan hapa nchini
Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu
jijini Dar es Salaam. |
Rais wa Jamhuri ya Muungano waTanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kulia akiagana na Balozi wa Japan Nchini Mheshimiwa Masaharu Yoshida mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu jijini Dar es Salaam. Picha na IKULU.
No comments:
Post a Comment