POLISI mkoani Arusha inamshikilia askari wake, PC
Rafael, maarufu kwa jina la Osama, kwa tuhuma za kumbaka mwanafunzi wa kidato
cha sita, anayesoma shule ya sekondari ya Wasichana ya Korogwe.
Akizungumza kwa uchungu akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Arusha ya Mt. Meru, mwanafunzi huyo, ambaye jina lake limehifadhiwa, alisema mkasa huo ulimpata juzi wakati akielekea kwa ndugu yake anayeishi kwa Mrombo.
Kwa mujibu wa wanafunzi huyo, alitoka Mwanza kwa basi
la Kampuni ya Isamilo kwa lengo la kwenda shuleni Korogwe, na alipofika standi
kuu ya mabasi Arusha, alikata tiketi nyingine kwa ajili ya kwenda Tanga siku
iliyofuata.
“Baada ya kukata teketi, nilipanda daladala kwa ajili
ya kwenda kwa Mrombo, baada ya kushuka nikiwa kwenye daladala na kwenda mbele
kidogo, nilihisi kupotea, ambapo niliomba msaada kwa kijana mmoja ili anipe
simu niweze kuwasilina na ndugu zangu,” alisema.
Alidai wakati akipatiwa msaada wa simu, ghafla alitokea askari huyo wa Kikosi cha Kutuliza Ghasia (FFU), akiwa amevalia sare za kikosi hicho na kumuamuru kijana huyo amuache mwanafunzi huyo.
Alidai askari huyo alitoa kitambulisho na kumuonyesha mwanafunzi huyo, aliyekuwa amevaa sare za shule na kumwambia yupo kwenye mikono salama na kumtaka amfuate ili ampeleke Kituo cha Polisi cha Mbauda, aweze kupata msaada wa anakokwenda.
Alidai wakati wakiwa njiani, Osama alikuwa anasalimiana na watu mbalimbali, hali iliyomfanya mwanafunzi huyo kuamini kuwa yuko kwenye
mikono salama.
“Baada ya kutembea umbali mrefu, askari huyo aliniuliza kama namuamini, nikamjibu hapana na alitoa tena kitambulisho chake nikakisoma vizuri nikagundua anaitwa Rafael,” alidai.
Huku akionekana kuwa na majeraha makubwa usoni ya kupigwa, mwanafunzi huyo alisema polisi huyo alimuambia bado kidogo wafike kituo cha polisi na kumtaka wapite njia ya mkato kwa kuwa ilikuwa usiku wa saa mbili.
Alidai kadri walivyokuwa wanatembea, askari huyo alikuwa anaelekea kwenye pori nene, hali iliyompa wasiwasi na kumuuliza tena askari mahali wanakoelekea, ambapo alimjibu kuwa wanakaribia.
Alidai ghafla askari huyo alimpiga ngwara kisha kumweleza kuwa hapo ndipo kituo cha polisi,hali iliymfanya mwanafunzi huyo kupiga kelele za
kuomba msaada, lakini hakufanikiwa.

“Alinipiga teke la mdomoni, akaninyonga, halafu
akanipiga mateke mengine mgongoni na kuniamuru nivue nguo, lakini niligoma.
“Baada ya kukataa kufanya hivyo, askari huyo alinivua nguo kwa lazima kisha kuanza kunibaka kwa saa kadhaa mpaka nikapoteza fahamu,” alidai.
Aliongeza kuwa baada ya kupigwa na baridi alizinduka
saa tisa usiku na kumuona askari huyo akipekua begi lake dogo kisha kuchukua
fedha kiasi cha sh. 17,000, alizokuwa nazo kwa ajili ya karo ya shule na
nyingine za maandalizi ya mahafali yake yaliyokuwa yafanyike mapema Aprili,
mwaka huu.
Alidai baada ya askari huyo kuchukua fedha hizo na
kutokomea kusikojulikana, alijikokota kwa shida kutokana na maumivu aliyokuwa
nayo mpaka kituo cha mafuta, kilichoko karibu na eneo la FFU, ambapo aliomba
msaada kwa wahudumu.
Alidai baada ya kutoa kitambulisho cha shule, walimpa
mahali pa kulala kisha asubuhi kumpeleka kituo kikuu cha polisi ambapo,
aliandika maelezo na kupelekwa katika Hosptali ya Mkoa ya Mt. Meru kwa ajili ya
matibabu.
“Baada ya kukaa wodini kwa saa sita, nilipelekwa tena kituo cha polisi kwa ajili ya gwaride la utambuzi, ambapo nilikuta askari zaidi ya 10 na nikamtambua na alipotaka kubisha, niliwaomba wamkague kwenye mwili wake kuna sehemu nilimng’ata.

“Nimeumizwa sana, nimekatizwa masomo, muda huu
ningekuwa shuleni, naomba serikali inisaidie na mtuhumiwa wa ukatili huu
achukuliwe hatua,” alisema.
Mama mzazi wa mototo huyo, Hadija Hassan (45), ambaye alifika jana, akitokea Mwanza, alimuomba Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Ernest Mangu, kuchukua hatua kali za kisheria dhidi ya askari
wake wanaokiuka maadili ya kazi zao.

Mganga Mkuu wa Mt. Meru, Jackline Urioh, alikiri
kupokea mwanafunzi huyo akiwa katika hali mbaya na kwamba, baada ya kupata
matibabu anendelea vizuri kiasi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Lebaratus Sabas,
alisema kwa sasa hawezi kuzungumzia suala hilo hadi hapo uchunguzi wa awali
utakapokamilika.
No comments:
Post a Comment