Thursday, 21 January 2016
MCHUNGAJI ANASWA AKIZINI NA BINTI YAKE
MCHUNGAJI wa Kanisa la Evangelist Assemblies of God, Abel Godfrey, amekamatwa na waumini wake kwa tuhuma za kushiriki mapenzi na binti wa kaka yake.
Habari za kuaminika na zilizothibitishwa na ndugu na viongozi wa serikali ya kijiji, zimesema kuwa Mchungaji Godfrey, amekuwa na uhusiano wa kimapenzi na binti yake huyo mwenye umri wa miaka 20, ambaye ana mtoto wa miezi minne.
Tukio hilo limetokea juzi saa tano usiku, katika Kijiji cha Mgongoro wilayani hapa, ambapo kabla ya kumtia mbaroni, waumini na baadhi ya wananchi waliweka mtego na kufanikiwa kumnasa.
Akizungumza kwa masikitiko, babu wa binti huyo, Bictoni Kyarero, alidai mchungaji huyo amekuwa kwenye mahusiano hayo kwa zaidi ya mwaka mmoja sasa.
“Huyu Mchungaji ametusikitisha sana kwani ni jambo la aibu kufanya mapenzi na mtoto wa kaka yake huku akijua yeye ni kiongozi wa waumini. Pia ni jambo la fedheha kwa Mwenyezi Mungu kwa kuwa jambo kama hilo ni laana kubwa,’’ alidai babu wa binti huyo.
Aliendelea kufafanua kuwa, hata walipomkamata alijaribu kukimbia, lakini walimdhibiti huku akikiri kufanya mapenzi na binti wa kaka yake.
Kwa upande wake, binti huyo alipoulizwa juu ya kutembea na baba yake mdogo, alikiri kufanya hivyo na kusema, alitenda kosa hilo baada ya kuambiwa na mchungaji huyo iwapo angelikataa kufanya tendo hilo, angeombewa kwa Mungu ili awe kichaa.
Naye Mchungaji Godfrey alikiri kutenda kosa hilo na kudai kuwa ni ushawishi wa shetani na kuongeza kuwa hawezi kurudia tena kosa hilo.
Mtendaji wa Kijiji cha Mgongoro, Edward Kitenya, alisema kiongozi huyo wa kiriho alikiri kuhusika na kutozwa faini ya sh. 20,000 na kuachiwa huru.
Kwa upande wao, baadhi ya wananchi wameuomba uongozi wa kanisa hilo kumvua uongozi kwa kuwa amekiuka maadili ya uongozi na kufanya waumini kutomwamini tena.
Mtendaji wa Kata ya Igunga, Fredrick Masesa, amewaomba viongozi wa dini pamoja na wananchi kuzingatia maandiko matakatifu ya Mwenyezi Mungu ya kutofanya vitendo viovu.
Mchungaji wa Kanisa la Kijiji cha Mwanzugi, Fanueli Daniel, amethibitisha kukamatwa kwa mchungaji huyo na kueleza kuwa, tayari wamemsimamisha uchungaji kwa muda usiojulikana.
Alisema kuanzia sasa kanisa hilo litaongozwa na Philipo Makeremo, ambaye pia ni Katibu wa kanisa.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment