MKEMIA Mkuu wa Serikali, Profesa Samwel
Manyelle, ametoa ufafanuzi wa taarifa zinazohusu asilimia 47 ya watoto
wanaozaliwa hapa nchini kuwa si wa baba husika.
Akizungumza mjini Dar es Salaam,
juzi, Profesa Manyelle alisema, vyombo vya habari vilimnukuu vibaya kwa vile
asilimia hiyo ni ile ya maombi yanayowasilishwa ofisini kwake, sio nchi mzima.
Alisema asilimia 47 ya maombi
yanayowasilishwa katika ofisi yake kuchunguzwa, yalionekana kuwa na matokeo
hayo, na si kwamba yalihusu nchi nzima.
Profesa Manyelle alitoa ufafanuzi
huo, baada ya Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya
Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Hamis Kigwangalla, kumuuliza kuhusu ukweli
wa taarifa hizo, huku akitaka kujiridhisha juu ya vipimo vya kutambua vinasaba
(DNA), kubaini ukweli juu ya mtoto.
“Tulizungumzia kuhusu sampo zilizowasilishwa
ofisini kwangu, ambazo baada ya kuzifanyia uchunguzi, tulibaini matokeo hayo
kwamba, asilimia 45 za sampo hizo,
watoto walionekana si wa baba husika,” alisema Profesa Manyelle.
Kutokana na ufafanuzi huo, Dk. Kigwangwalla
alikanusha taarifa hizo zilizokuwa zimeenea na kwamba ziliwadhalilisha wanawake
kwa sababu zilitoa picha tofauti.
No comments:
Post a Comment