Saturday, 12 March 2016
NORWAY YAIPATIA TANZANIA SHILINGI BILIONI 2.6
TANZANIA imepokea msaada wa sh. bilioni 2.6 kutoka Serikali ya Norway, ambazo zimelenga kuinua kilimo nchini kupitia Mpango wa Uendelezaji Wakulima Wadogo katika Ukanda wa Kusini mwa Tanzania (SAGCOT).
Katibu Mkuu wa Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Dk. Florence Turuka, alisema hayo jana, wakati wa uzinduzi wa mpango huo na kwamba, fedha hizo zitatumika kuboresha teknolojia ya kilimo.
“Serikali itasaidia kutimiza malengo yaliyowekwa katika mpango huu ili pia iweze kutimiza malengo ya milenia ya kufika katika uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025,” alisema.
Alisema zipo jumla ya sekta binafsi 15, zinazosaidia wakulima katika harakati za kuinua sekta hiyo nchini.
Kwa mujibu wa Dk. Turuka, suala hilo ni muhimu kwa kuwa serikali haijihusishi moja kwa moja na biashara ya mazao.
“Tumekuwa tukilazimika kununua mazao kupitia Wakala wa Chakula wa Taifa (NFRA), lengo likiwa ni kuwainua wakulima wasikose soko na pia kuweka chakula cha akiba kitakachosaidia pindi unapotokea upungufu,” alisema.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Abbas Kandoro, alisema Tanzania hususani mkoa wa Mbeya, unafanya vizuri katika kilimo kupitia mpango wa ‘Kilimo Kwanza’, licha ya changamoto mbalimbali.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment