WAKUU wa Mikoa na Wakurugenzi wa Halmshauri nchini,
wametakiwa ifikapo Machi 30, mwaka huu, wawe wamewasilisha taarifa za watumishi
hewa kwenye vituo vyao vya kazi ili zikabidhiwe kwa Rais Dk. John Magufuli.
Hatua hiyo ni mkakati wa serikali kuhakikisha watumishi
hewa wanaondolewa ili kuokoa fedha zinazotumika kuwalipa mishahara.
Agizo hilo lilitolewa jana na Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais TAMISEMI, Geogre Simbachawe, wakati akizungumza na gazeti hili, kuhusiana
na juhudi zinazofanywa na wizara yake kumaliza uwepo wa watumishi hewa, hususan
kwenye halmashauri mbalimbali nchini.
Alisema tayari ameshawaandikia barua wakuu wa mikoa na wakurugenzi
wa halmashauri ili kuwasilisha ofisini kwake, orodha ya watumishi hewa ili
ikabidhiwe kwa rais kwa hatua zaidi.
Alisema mishahara hewa ni wizi unaofanywa na baadhi ya
watendaji wa serikali, ambao sio waaminifu, hivyo amewataka wakurugenzi na
waweka hazina wa halmashauri zote kumaliza tatizo hilo haraka iwezekanavyo.
“Tutahakikisha
tatizo hilo tunalikomesha mara moja ili kuhakisha tunaokoa fedha nyingi za serikali zilizokuwa zinapotea,’’ alisema.
Alisema tatizo la
watumishi hewa na mishahara haliko kwa
walimu tu, bali kwa watumishi wengi wa serikali.
Katika
hatua nyingine, Mwandishi Wetu, Rhoda Ezekiel, ameripoti kutoka Kigoma kuwa,
Mkuu wa mkoa huo, Brigedia Jenerali mstaafu Emanuel Maganga, amewataka wakuu wa
wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za mkoa, kuhakikisha wanafanya uchunguzi
juu ya kiasi cha fedha kilichotumika kuwalipa mishahara watumishi hewa 169, kwa
kipindi cha mwaka mmoja uliopita.
Akizungumza
na waandishi wa habari, jana, Maganga alisema ametoa agizo hilo ikiwa ni
itekelezaji wa agizo la Rais John Magufuli la kufanya uhakiki wa watumishi
katika halmashauri zote nchini, ili kuwabaini watumishi hewa wanaolipwa
mishahara kinyume na taratibu za utumishi.
Alisema
kati ya watumisho hao 169, waliowabaini kuwa ni hewa, wapo ambao walishafukuzwa
kazi, waliokwishafariki na wengine hawana sifa za kuwa watumishi wa umma.
Maganga
alisema suala la kuwa na wafanyakazi hewa ni wizi, ambao hauwezi
kuvumilika na pia ni wizi wa kuibia wanyonge hivyo hauwezi kuvumilika.
"Hakuna
anayeweza kuvumilia wizi wa waziwazi kiasi hiki unaofanywa na baadhi ya
watumishi wasio waaminifu, wale wote watakaobainika wajiandae kwani hatua za
kisheria zitachukuliwa dhidi yao," alisema.
Alisema
fedha walizokuwa wakilipwa watumishi hao hewa kwa ajili ya mishahara,
zinatakiwa kurudi zote na pia wakurugenzi wawafute watumishi hao hewa kwenye
orodha ya malipo.
Mkuu
huyo wa mkoa alisema katika serekali ya awamu ya tano, hakuna kufanyakazi kwa
mazowea na uzembe na kwamba, kila mtumishi atumike kwa nafasi yake aliyopo.
Alizitaja
halmashauri zenye watumishi hewa kuwa ni Kasulu (78), Kigoma (23), Manispaa ya
Kigoma Ujiji (29), Buhigwe (11), Uvinza (19), Kibondo (5), ofisi ya mkuu wa
mkoa (4).
No comments:
Post a Comment