Friday, 1 July 2016

MKE WA RAIS,MAMA JANETH MAGUFULI AMKARIBISHA MGENI WAKE MKE WA RAIS WA RWANDA MAMA JANETH KAGAME OFISINI KWAKE LEO

Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kushoto) akiwapungia wananchi wakati alipomkaribisha Mke wa Rais wa Rwanda Mama Janeth Kagame katika Ofisi zake wakati wa Ziara ya Rais wa Rwanda, Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisaini kitabu cha wageni wakati alipotembelea ofisi za mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mama Janeth Magufuli mapema hii leo jijini Dar es Salaam ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame hapa nchini.

Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) akisikiliza kwa
makini shughuli mbalimbali zinazofanywa na ofisi ya mke wa Rais MamaJaneth Magufuli wakati alipotembelea ofisi hizo ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiwa katika picha ya pamoja na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Janeth Magufuli (kulia) akiagana na mgeni wake Mke wa Rais wa Rwanda Bi. Janeth Kagame (kushoto) mara baada ya Mama Kagame kutembelea ofisi za Mama Magufuli ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya Rais wa Rwanda Paul Kagame mapema hii leo jijini Dar es Salaam.Picha na Benjamin Sawe - Maelezo

No comments:

Post a Comment