Monday, 18 April 2016

JAJI MKUU OTHMAN CHANDE AKUTANA NA JAJI WA MAHAKAMA KUU YA CHINA

Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang ( kushoto) akiagana na  Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (kulia) mara baada ya kukutana na kufanya mazungumzo naye leo jijini Dar es salaam. Picha/Aron Msigwa.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (wa pili kutoka kushoto mbele) akiwa katika picha ya pamoja na Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman (katikati) na baadhi ya watendaji wa Mahakama ya Tanzania mbele ya Jengo la Mahakama ya Rufaa leo jijini Dar es salaam.
Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Tanzania Mhe. Shaban Lila(kulia) akimweleza jambo jaji wa Mahakamu Kuu ya Jamhuri ya Watu wa China mara baada ya kumkaribisha Ofisini kwake Mahakama Kuu leo jijini Dar es salaam.
Jaji wa Mahakama Kuu ya Watu wa Jamhuri ya China, Mhe. Zhang (kushoto) akipokea zawadi ya kinyago kutoka kwa Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohammed Chande Othman.


Na Mwandishi- Mahakama ya Tanzania

Jaji Kiongozi wa Mahakama ya Juu Nchini China Mheshimiwa Zhang Jiannan yuko Nchini kwa ziara ya kikazi yenye lengo la kuimarisha uhusiano na ushirikiano uliopo baina ya nchi za Tanzania na China.

Katika ziara yake Nchini, Mheshimiwa Jiannan ambaye anamwakilisha Jaji Mkuu wa China, leo alikutana na Jaji Mkuu wa Mahakama ya Tanzania Mheshimiwa Mohamed Chande Othman na kubadilishana uzoefu wa utendaji kazi wa Mahakama zao.

Akizungumzia changamoto za Mahakama nchini China, Mheshimiwa Jiannan alisema hivi sasa Mahakama za China zinakabiliwa na upungufu wa Majaji ikilinganishwa na idadi ya kesi zinazosajiliwa.

Kwa Upande wake, Jaji Mkuu wa Tanzania alisema baadhi ya changamoto zinazoikabili Mahakama ya Tanzania ni pamoja na upungufu wa Mahakama za mwanzo.

Alisema ili kukabiliana na upungufu huo, Tanzania inahitaji kuwa na Mahakama za Mwanzo 3000 nchi nzima. Hivi sasa kuna Mahakama za Mwanzo karibu 960 nchini kote ambazo hazitoshi ikilinganishwa na Idadi ya kata zilizopo Nnchi mzima.Jaji Mkuu wa Tanzania alimshukuru Jaji Mkuu Kiongozi wa China kwa kuitembele Mahakama ya Tanzania.

Katika ziara yake nchini, Jaji Jiannan ameongoza ujumbe wa Majaji na Watendaji wengine wa Mahakama wanne kutoka nchini China.

No comments:

Post a Comment