Wednesday, 31 August 2016
JWTZ SASA KUTOKA KIVINGINE KESHO
NA CHRISTOPHER LISSA
JESHI la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ), limewataka wananchi kutokuwa na hofu wakati litakapokuwa linaadhimisha kilele cha miaka 52 ya kuanzishwa kwake kesho.
Badala yake, JTWZ limewataka wananchi kuungana bega kwa bega katika kushiriki kikamilifu kwenye
shughuli za maendeleo na kijamii
zitakazofanywa na vikosi vyake.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, wakati wa hafl a ya kumkabidhi ratiba ya maadhimisho hayo Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, Msemaji wa JWTZ, Kanali Ngemela Lubinga, alisema wamejipanga kikamilifu kuadhimisha siku hiyo muhimu.
Alisema JWTZ itarusha ndege zake angani, hivyo kuwataka wananchi kutokuwa na hofu.
ìNdege zitapita angani kwa ajili ya kutoa heshima na utii kwa wananchi wake ambao walilianzisha jeshi na wanaliamini,îalisema Kanali Ngemela.
Aidha, kutakuwa na maonyesho mbalimbali ya kijeshi ya JWTZ, ambapo wananchi wametakiwa kushiriki kikamilifu.
Kanali Ngemela alisema katika
kambi zake, wanajeshi wamekuwa wakijifua kwa muda mrefu ili kuhakikisha kwamba siku ya maadhimisho hayo, Septemba Mosi, mambo yanakwenda kama yalivyopangwa.
Alisema pamoja na shughuli nyingi
za kijeshi ambazo zinatarajiwa kufanyika, pia vikosi vya JWTZ vitatawanyika katika maeneo mbalimbali nchini kufanya shughuli za usafi na upandaji miti.
ìWanajeshi watakuwa wakichangia damu kwa ajili ya kuokoa maisha ya watu. Vijana wetu wako tayari na wana afya njema kwa ajili ya kuchangia damu kwa kuwa tatizo la damu ni kubwa,îalisema Kanali Lubinga.
Kutokana na maagizo ya serikali, vikosi vya JWTZ vitashiriki kikamilifu katika suala la usafi mitaani na upandaji miti.
“Usafi ni afya, vilevile ni amani. Bila usafi afya haipo na amani haipo kwa sababu wananchi watapoteza maisha,” alisema kanali huyo.
Alisema madaktari wa JWTZ watasambazwa katika vituo mbalimbali wakitoa huduma za ushauri nasaha, kupima kisukari na shinikizo la damu.
“JWTZ itashiriki kikamilifu katika
michezo kama sehemu mojawapo ya shughuli za wanajeshi na utimamu wa wanajeshi,” alibainisha Kanali Lubinga.
Msemaji huyo aliwataka wananchi kushirikiana na jeshi hilo kwa kuwa jeshi hilo ni mali ya wananchi wa Tanzania.
Alisema shughuli za maadhimisho
hayo zilianza wiki iliyopita, ambapo shughuli za kijeshi zinaendelea, ikiwa ni pamoja na kupiga kwata, mafunzo na kufanya kumbukumbu ya shughuli za ulinzi wa amani nje na ndani ya nchi.
Kwa upande wake, Makonda
alilipongeza jeshi hilo kwa kulinda amani, hivyo kuwataka wakazi wa Dar es Salaam kuungana na JWTZ hapo
kesho.
“Kama kuna mwananchi au kuna kikundi kinataka kushirikiana na JWTZ
katika shughuli mbalimbali hapo
kesho, basi wawasiliane na wakuu wa wilaya ili wapangiwe maeneo,” alisema
Makonda.
Akizungumzia tishio la
maandamano batili ya Ukuta, Makonda alisema Septemba Mosi ni siku ya maadhimisho ya JWTZ na wananchi waelewe hivyo.
“UKUTA ni kiwango cha mwisho cha mtu kufi kiri. Ukisikia msemo wa Kiswahili unaosema amegonga ukuta, maana yake akili zake zote zimeisha. Sisi akili tunazo, hatuwezi kuongelea watu ambao wamefi kia mwisho wa kufi kiri,” alisema Makonda.
Aliongeza kuwa: “Septemba Mosi tunaelewa maana ya maadhimisho ya JWTZ, lakini ukikumbuka pia Septemba Mosi hiyo ilikuwa ni Siku ya Mashujaa, hivyo ni siku muhimu. Hao waliogota kufi kiri hatuna sababu ya kuwalazimisha kufi kiri zaidi ya kuwaonyesha maana ya kufi kiri kwa vitendo.”
KIONGOZI NCCR-MAGEUZI AONYA
Katika hatua nyingine, Jacqueline Massano Mageuzi, Leticia Mosore, amesema maandamano siyo njia pekee ya kutatua matatizo ya vyama vya siasa nchini na badala yake watafute njia ya maridhiano na serikali.
Amesema kazi ya vyama vya upinzani si kupingana na serikali iliyopo
madarakani, bali ni kuikosoa kwa hoja za msingi na zenye maslahi kwa taifa.
Akizungumza na waandishi wa habari jana mjini Dar es Salaam, Leticia alisema wanasiasa wanapaswa kujenga utamaduni wa kuheshimu viongozi waliopo madarakani.
“Tunahitaji kukaa chini, kutafakari na kujipanga jinsi ya kufanya siasa za ushindani katika kipindi hiki na
zitakazolisaidia taifa, kwa kutumia lugha za staha katika kufi kisha ujumbe.
“Kama hatuna cha kukosoa ni bora tukanyamaza na kupanga mikakati ya kujenga vyama vyetuÖsiyo lazima tuseme ili tuonekane tunasema, hata kama tunayosema hayana maslahi kwa Watanzania walio wengi,” alisema Leticia.
Aliongeza kuwa bado kuna fursa kwa vyama hivyo kujadiliana jinsi ya kuendesha siasa, kuliko kuendelea kupambana kwa maneno yasiyo na tija.
“Haiwezekani jamii na viongozi wa dini nchini wanamwombea Rais, Dk. John Magufuli, halafu sisi viongozi wa UKAWA twende mitaani na kwenye mikutano ya hadhara tuseme Rais Dk. Magufuli ni dikteta, hafuati Katiba na aheshimu sheria, anawanyanyasa wafanyabiashara wanaokwepa kodi, anawatumbua waliotuhumiwa na ufi sadi, halafu wananchi watuelewe,” alisema Leticia.
Hata hivyo, alivitaka vyama hivyo kuacha kuichonganisha serikali na
wananchi kwa sababu wanarudisha nyuma jitihada zinazofanywa na Rais mwenye dhamira ya dhati ya kuiletea neema Tanzania.
“Tuachane na mikutano ya kuchochea na kujenga chuki dhidi ya serikaliÖWatanzania wanauelewa na ufahamu mkubwa wa kupambanua mambo,” alisema.
Kiongozi huyo wa NCCR – mageuzi alitoa wito kwa vijana kuacha kuchukiana kwa sababu kila mmoja ana haki ya kuwa katika chama anachoona kinamfaa.
“Haiwezekani muda wote, miaka yote iwe ni ya kufanya siasa kuanzia asubuhi hadi jioni. Hivi sasa muda mwingi utumike kujijenga kiuchumi na kufanya siasa kwa mpango maalum.” aliasa.
Hata hivyo, alisema kwa sasa UKAWA imepoteza mweleko kutokana na kushindwa kuendana na kasi ya Rais Dk. Magufuli.
“Kiukweli wote tulisubiri mabadiliko na ukweli Watanzania tulihitaji mabadiliko, tunashukuru Mungu yale yote tuliyokuwa tunayapigia kelele kuhusu rushwa na ufi sadi, uzembe na ukwepaji kodi yanafanyiwa kazi kivitendo,” alisema.
Alisema UKAWA kwa sasa imekuwa ni umoja wa wafanya vituko bungeni kutokana na kususia vikao
vya Bunge na kutoka nje huku wakiwa wamefunga midomo.
MAANDAMANO UKUTA HAYAFANYIKI
Katika hatua nyingine, JONAS KAMALEKI wa MAELEZO anaripoti kuwa maandamano ya Ukuta hayawezekani, kwani hii ni ndoto ya mchana na hayana msingi wowote wala tija kwa wahusika hata kwa taifa, imeelezwa.
Hayo yalisemwa na Mhadhiri Mwandamizi wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM) Profesa Benson Bana.
“Wanaotaka kuandamana wanajidanganya na kuwalaghai wenzao, kwani kufanya operesheni ni suala la dola na si la mtu au kikundi cha watu, hivyo maandamano hayo hayawezekani kabisa,” alisema Profesa Bana.
Aliongeza kuwa: “Wanaojiita Ukuta ni kwamba Rais Dk. Magufuli amewanyima ajenda kwani utendaji wake umezidi fahamu zao na kuwafanya waanze kutapatapa wasijue nini la kufanya.”
Profesa Bana alisema kama viongozi
wa Ukuta ni waungwana, inabidi watamke wazi kuwa wametafakari na kuona maandamano hayana maana, hivyo wameamua kuyasitisha nchi nzima.
Kuhusu utendaji wa serikali, Profesa. Bana alisema ni serikali yenye uamuzi wa uhakika na inayowajali wananchi bila kujali itikadi zao za vyama, dini wala makabila.
“Rais Magufuli utendaji wake ni wa kuigwa na viongozi wengi duniani kwani anafanya uamuzi wa uhakika, ikiwemo kukuza uchumi kwa kukusanya kodi na kuziba mianya ya ubadhirifu wa mali ya umma,” alisema Profesa Bana.
“Pamoja na kuwa Rais Magufuli amekuwa madarakani kwa kipindi kifupi, viashiria vyote vinaonyesha ni kiongozi imara na shupavu kutokana na mambo makubwa ambayo aliyoyafanya kwa kipindi hiki kifupi,” alisisitiza.
Aliongeza kuwa: “Kumekuwepo na nidhamu katika utumishi wa umma, kodi inakusanywa kwa kiwango kikubwa na elimu ya msingi inatolewa bure kama Ilani ya Uchaguzi ya Chama tawala inavyosema.”
Profesa Bana alisema
wanaomlaumu rais ni wale ambao hawajitambui na labda wanaona mianya ya ubadhirifu anayoendelea kuziba, wao wanakosa mapato.
UVCCM MWANZA WALAANI
Kutoka Mwanza, Peter Katulanda anaripoti kuwa Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM)
mkoani Mwanza, umelaani wanasiasa wanaoendelea kushinikiza maandamano haramu ya Ukuta yanayoashiria uvunjifu wa amani nchini.
Umesema vijana watakaofuata mkumbo wa wanasiasa hao kwa kulazimisha kuandamana, waache tabia hiyo.
Hayo yalisemwa jana na Katibu wa UVCCM Mkoa wa Mwanza, Elieza Philipo, wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu mwenendo wa kauli za kushinikiza maandamano hayo.
“Hakuna haki yoyote duniani
isiyokuwa na wajibu. Moja ya wajibu huo ni kutii sheria bila shuruti, nawaasa vijana wenzetu waelewe hakuna uhuru wa kufanya lolote duniani bila kuwepo kwa mipaka,” alisema.
Philipo aliongeza kuwa: ìTunawalaani vijana watakaofuata mkumbo wa maandamano hayo haramu na tunaomba Watanzania wengine wawalaani wote wanaotaka kutuvurugia amani nchini kwa ajili ya maslahi yao binafsi.î
MACHINGA WAMTAKA
JPM KUWA NA AMANI
Wafanyabiashara ndogo maarufu kama machinga katika maeneo
mbalimbali jijini Dar es Salaam, wameapa kutoshiriki katika maandamano batili ya Ukuta na kumtaka Rais Dk. Magufuli, kuwa na amani ofi sini kwake Ikulu, anaripoti Christopher Lissa.
Pia, wafanyabishara hao wamewataka wenzao kote nchini kufungua biashara zao kama kawaida, kisha kupuuza ushawishi wa kwenda katika maandamano hayo ambayo
wamedai hayana tija kwao na kwa taifa.
Wakizungumza katika mkutano ulioitishwa na Umoja wa wana Machinga eneo la Mwenge, Dar es Salaam,jana, wafanyabiashara hao walisema hawako tayari tena kutumika na wanasiasa wa vyama vya upinzani, kwani wana imani na Rais Dk. Magufuli ambaye amesikiliza kilio chao na ni
mtetezi wa haki za wanyoge.
Mwenyekiti wa Umoja wa Wafanyabishara hao Mwenge, Omari Khamis, alisema uamuzi huo wameufi kia baada ya kuridhika kwamba serikali inafanya jitihada kubwa za kuwaletea wananchi maendeleo bila kujali itikadi zao na kutetea wananchi wanyonge.
“Kunapotokea jambo lolote la hatari, sisi wafanyabisha wadogo, mama lishe, bodaboda na waendesha bajaji,
tumekuwa ndiyo mtaji wa wanasiasa wa upinzani kututumia katika kufanikisha
matakwa yao kisiasa, lakini awamu hii hatutakubali kushiriki katika jambo lolote
la Ukuta na kwa umoja wetu tunaomba wafanyabishara kote nchini wasikubali kutumika badala yake waendelee na bishara zao kama kawaida,” alisema Khamis.
Alisema ana amini wapo baadhi ya wafanyabishara ambao wanaweza kurubuniwa kwa fedha, lakini wafanyabishara hao kabla ya kupokea fedha hizo, watathmini amani ya taifa, familia zao na maisha yao.
“Tunamhakikishia Rais wetu Dk. Magufuli kwamba kesho awe na amani ofi sini kwake Ikulu…aendelee na majukumu yake kama kawaida ya kuwapigania wananchi wanyonge na kujenga uchumi wa taifa letu. Vijana wake machinga tupo hapo kesho tutakuwa imara na msimamo wetu kuhakikisha tunapinga maandamano
hayo ili taifa letu liwe na amani,” alisema Khamis.
Katika Soko la Karume, pia machinga walidai kamwe hawako tayari kushiriki kitu chochote kinachoitwa maandamano.
“Tutakachofanya ni kufungua biashara zetu kama kawaida. Tunachoomba wajipitie na maandmano yao watuache tukifanya biashara zetu, ole wao wakipita na maandamano halafu wazikanyage bidhaa zetu,” alionya mfanyabiashara ambaye aliomba jina lake lihifadhiwe.
Kwa upande wa Kariakoo, machinga walisema hakuna litakalotokea kwani wako na Rais Dk. Magufuli ambaye amekuwa akiwapigania.
Aidha wafanyabishara hao wamewatoa hofu wateja wao juu ya maandamano hayo na kuwahakikishia usalama mwanzo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment