Thursday, 4 May 2017

MAALIM SEIF: LIPUMBA NI MSALITI, HERI KUKAA MEZA MOJA NA CCM



Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad kupitia Clouds 360 ya Clouds TV amedai kuwa bora akae na CCM kuliko kukaa na Mwenyekiti wa CUF anayetambulika na Msajili wa Vyama vya siasa Prof. Ibrahim Lipumba kwa kuwa ni msaliti.

Akijibu swali la mtangazaji wa kipindi hiko Masoud Kipanya aliyeuliza kama anaweza kukaa Ofisi moja na Prof. Lipumba, Maalim Seif alijibu: “Siwezi, siwezi kukaa na msaliti. Ni bora kukaa na CCM kuliko kukaa na msaliti.” – Maalim Seif.

Prof. Lipumba alikuwa mmoja wa watu waliomkaribisha Lowassa kujiunga na UKAWA kwa kuwashawishi viongozi wa Muungano huo wampokee na kupendekeza jina la muungano huo.

Awali, Maalim Seif alisema kuwa Lipumba ndiye aliasisi jina la UKAWA akisema: “Prof. Lipumba ndio alitoa jina la UKAWA.

Kisha baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania Edward Lowassa kukatwa jina lake katika kugombea Urais kupitia CCM alikaribishwa UKAWA na Prof. Lipumba akisema: “Baada ya Lowassa kukatwa na CCM, Prof. Lipumba ndio alimkaribisha UKAWA na kuwashawishi viongozi wa UKAWA wampokee.

Na alipoulizwa kuhusu kujiuzulu kwa Prof. Lipumba kisha kurudia tena katika wadhifa wake ndani ya CUF, Maalim Seif alisema: “Prof. Lipumba alijiuzulu, na Katiba ya CUF hairuhusu kitendo cha ‘kutengua’ kujiuzulu kwake.

Aidha, Makamu huyo wa Kwanza wa Serikali iliyopita ya Mapinduzi Zanzibar aliongeza kwa kusema kuwa Prof. Lipumba na kundi lake wanafanya uhalifu kuzikalia Ofisi za CUF: “Prof. Lipumba na kundi lake ambao wamekalia Ofisi za CUF, sio wanachama wa CUF na hivyo wanafanya uhalifu kukalia Ofisi hizo.” – Maalim Seif.
IMETOLEWA KUTOKA MILLARDAYO

No comments:

Post a Comment