Na Mwandishi Wetu, Musoma
KUJITOKEZA kwa
mgombea ubunge wa jimbo
la Musoma Mjini kupitia ACT Wazalendo,
Eliud Tongoara (Mkorea) kumesabisha mpasuko mkali ndani ya
CHADEMA, hatua ambayo imesababisha zaidi ya wanachama
na mashabiki 3,800 kukihama chama hicho na kujiunga
na CCM katika mikutano mitatu ya CCM.
Wanachama hao na mashabiki
wajiunga na CCM kwa nyakati tofauti, katika mikutano
ya uzinduzi wa kampeni za CCM, ambayo ilifanyika
viwanja vya shule ya Sekondari ya Mara, Kata
ya Nyamatare, Bweri na Kata ya Nyasho mjini
mjini hapa.
Baadhi ya wanachama
hao wakizungumza wakati wakijiunga na CCM), walidai kutoridhishwa na
mchakato wa mgombea ubunge wa Chadema, Vicent Nyerere, kwa kumuengua Eliud
Tongora, ambaye alilazimika kujiunga na ACT Wazalendo.
“Kwa vile baadhi
ya viongozi wa Chadema walitanguliza ubinafsi na chuki
kwa kumuengua ‘Mkorea’, sasa na sisi tumeamua kuingia CCM
ili tuone wao walimwaga mboga, sisi tumemwaga ugali, tuone nani
mshindi,” alisema Magafu Willison, mkazi wa Nyasho.
“Tumeamua kujiunga na CCM na si
ACT Wazalendo ili tusionekane tumemfuata Mkorea, sasa tunajiunga na
CCM na tutahakikisha hakuna kulala hadi ushindi unapatikana,” alisema Pendo
James, mkazi wa Mwisenge.
Akihutubia katika
mkutano wa kampeni katika viwanja vya kituo cha mabasi
Nyasho, mgombea ubunge wa CCM, Vedastus Mathayo, alitangaza
kutoa sh. milioni 200 kwa kila kikundi
cha wanawake huku
vikundi vya vijana
vikiwezeshwa sh. milioni 50 kama
mitaji ya biashara, ikiwa ni
moja ya mkakati
wake wa kupambana
na umasikini kwa
wananchi wa jimbo
hilo kwa vitendo.
Mathayo, ambaye
pia ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa (NEC) ya CCM, alisema
amepanga kupambana na
umasikini kwa vitendo kwa
kuwataka vijana na wanawake kuunda
vikundi hivyo ili kuwezeshwa
mitaji hiyo kuanzia Januari,
mwakani.
Alisema kwa
sasa taratibu maalumu
zinandaliwa katika kusaidia
makundi mengine katika
jamii yakiwemo ya wazee.
Alisema endapo atachaguliwa
katika uchaguzi wa Oktoba 25, mwaka huu, suala la kupambana na
umasikini kwa wananchi wa jimbo la Musoma Mjini ni la kufa na kupona,
ikiwa ni pamoja na kubuni mikakati mipya ya kupambana na ajira kwa
vijana.
“Nimepanga kuanzia Januari, mwakani,
tuanzishe kambi maalumu ya vijana bila kujali itikadi za vyama vyao kwa ajili
ya kuwapa mafunzo maalumu ya ujasiriamali, ufundi na ujuzi mwingine ili baada
ya kuhitimu waweze kupatiwa mitaji na kujiajiri wenyewe,” alisema Mathayo.
Mathayo amewataka
wananchi wa jimbo la Musoma Mjini,
kufanya uamuzi kwa kupima
maendeleo, ambayo yamefanywa
wakati jimbo hilo, likiongozwa
na mbunge wa CCM katika
kipindi cha mwaka 2005-2010
na 2010-2015 wakati likiongozwa na upinzani badala
ya kupiga kura kwa
ushabiki wa kisiasa.
No comments:
Post a Comment