Sunday 6 December 2015

SIKU 30 ZA RAIS MAGUFULI MADARAKANI, AMEOKOA SHILINGI TRILIONI MOJA



Rais John Magufuli jana alitimiza mwezi mmoja tangu alipoapishwa kushika wadhifa huo huku akiweka rekodi ya kuokoa kiasi cha Sh 997.4 bilioni (karibu Sh 1trilioni) ambazo zilikuwa zitumike kwa matumizi yasiyo ya lazima na ukwepaji kodi.

Sh997.4 bilioni zilizookolewa zitaweza kutumika kununua magari ya wagonjwa, kujenga zahanati, kujenga barabara za lami, kununua madawati, kujenga vyumba vya madarasa, kuchimba visima, kununua mashine za uchunguzi wa magonjwa, magari ya wanafunzi, pikipiki kwa maofisa kilimo, mikopo ya elimu ya juu au kujenga viwanja vya michezo kadri Serikali itakavyoelekeza.

No comments:

Post a Comment