Saturday, 2 January 2016
WALIMU WAKUU SHULE ZA MSINGI WAWEKWA KIKAANGONI
NA REHEMA MAIGALA
SERIKALI imesema itaanza kuwawajibisha walimu wakuu wa shule za msingi, ambao wanafunzi wake watakaofika darasa la pili watakuwa hawajui kusoma na kuandika.
Imewataka wakaguzi wa shule hizo waende wakafanye ukaguzi ili kufahamu maendeleo ya wanafunzi na si kuangalia majengo.
Kauli hiyo ilitolewa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, alipotembelea Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dar es Salaam.
Alisema ni aibu kuona mwanafunzi anamaliza darasa la saba hajui kusoma na kuandika.
Profesa Joyce aliwataka walimu wakuu kuwa makini katika kuangalia maendeleo ya wanafunzi wao, hasa kuanzia madarasa ya chini.
“Kuanzia sasa, mwanafunzi akifi ka darasa la pili hajui kusoma na kuandika, mwalimu mkuu atawajibishwa kisheria," alisema.
Pia, aliwataka wakaguzi waende shule wakakague madaftari ya wanafunzi, ili kujua wanachofundishwa na maendeleo yao kwa ujumla.
Hata hivyo, Profesa Joyce aliitaka TET iandae mwongozo maalumu kwa wakaguzi wa shule, ili wanapofi ka wajue kazi za kufanya.
Alisema ubadilishaji wa mitaala mara kwa mara unasababisha wanafunzi wasifanye vizuri katika mitihani yao, hivyo kuna umuhimu mkubwa wa kuwashirikisha walimu wa ngazi zote katika uandaaji wa mitaala mipya.
Naye, Kaimu Mkurugenzi wa TET, Dk. Leonard Akwilapo, ambaye juzi aliteuliwa na Rais Dk. John Magufuli, kuwa Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu, Sayansi, Teknlojia na Ufundi, alisema wanajitahidi kufanya kazi kwa ufanisi kinachowakwamisha ni ufi nyu wa bajeti kutoka serikalini.
“Serikali iongeze bajeti ya elimu ili kazi zaidi ziweze kufanyika katika kuinua elimu ya Mtanzania,” alisema.
Wakati huo huo, Waziri alipotembelea Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) na kuutaka uongozi wa baraza hilo uwe makini katika suala la usajili wa vyuo.
Alisema vyuo vingi vinavyosajiliwa hivi sasa ni kwa ajili ya kufanya biashara na si kutoa elimu inayotakiwa. “Sekta ya elimu si biashara kama biashara mnazozifi kiria… msiwapotezee muda vijana kujiunga na vyuo ambavyo si makini,” alisema.
Profesa Joyce alisema kila chuo kinachojengwa ni lazima kiwe na maabara inayotumika na si maabara hewa kama zilivyo katika baadhi ya vyuo vingine.
Hata hivyo, Profesa Joyce alitoa mwezi mmoja kwa Katibu Mtendaji wa NACTE Dk. Primius Nkwera, kuvichunguza vyuo vyote na kujua ubora wake.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment