Saturday, 2 January 2016
RC TANGA AAMUA KUJILIPUA
NA SOPHIA WAKATI, TANGA
MKUU wa Mkoa wa Tanga, Mwantumu Mahiza, amesema yuko tayari kupoteza maisha, ama kukosa kazi kwa kuyashughulikia majina 16 ya vigogo wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya.
Amesema ameanza mpango mkakati wa kuwashughulikia vigogo hao na wasafi rishaji wa magendo wanaotumia bandari bubu zilizopo mkoani Tanga.
Pia, alisema katika majina hayo, wapo baadhi ya viongozi na watu mashuhuri na kwamba hatawaonea aibu wala kuwafumbia macho.
Mwantumu alisema baadhi ya wafanyabiashara wanapitisha magendo kwa nia ya kukwepa kulipa kodi kwa kutumia mwambao wa Bahari ya Hindi na maeneo mbalimbali ya mkoani hapa.
Alisema hayo jana ofi sini kwake na kuongeza kuwa ameanza kazi ya kupambana na watu wanaojihusisha na dawa za kulevya, baada ya kufanya tathmini na kujiridhisha.
Alisema vijana zaidi ya 867 mkoani humo wameathirika na utumiaji wa dawa hizo, hivyo njia pekee ya kuwanusuru vijana hao ni kusambaratisha mtandao wa wauzaji wakubwa wanaoingiza dawa hizo.
“Hatuwezi kwenda kwa kuachia biashara hizi za dawa za kulevya kwa ajili ya kupoteza nguvu kazi ya taifa, vijana hawa hata ukiwapeleka kwenye vituo vya 'Soubar House' wakitoka hawawezi kufanya kazi zozote za uzalishaji, hivyo hatupo tayari kuzalisha mazezeta tukiwa tunaona,” alisema.
Alisema takwimu ya vijana walioathirika kwa ulaji wa dawa hizo, haiwezi kuachwa hivi hivi na badala yake mkoa umeweka mkakati wa kuhakikisha unawakamata waingizaji wote waliopo mkoani hapa na kuwafi kisha kwenye vyombo vya sheria.
Hata hivyo, Mwantumu alisema kuzagaa kwa sukari kutoka nchini India katika maeneo ya mkoa huo, hakutoi fursa kwa viwanda vilivyo nchini, kutokana na baadhi ya watu wachache kuingiza sukari na kukwepa ushuru wa serikali.
Mwantumu alisema hawezi kufumbia macho suala hilo, kwani linaathiri uchumi wa nchi na kuikosesha mapato serikali. Mkuu huyo wa mkoa alisema ameanza kuandaa utaratibu wa kukamilisha ushahidi wa kutosha ili kuwafi kisha mahakamani watu hao.
“Nimefuatilia kwenye bandari zote bubu, nimepata majina ya wafanyabiashara ambao wanaendesha biashara za magendo hapa Tanga, sukari kutoka India na dawa za kulevya kwa kutumia usafi ri wa boti,” alisema.
Alisema inasikitisha kuona bidhaa za magendo madukani zimezagaa kila kona na kwamba kitendo hicho hakikubaliki kwa kuwa kufanya hivyo kunaikosesha serikali mapato na kudorora kwa bidhaa zinazozalishwa nchini.
Akizungumzia biashara ya dawa za kulevya, mkuu huo wa mkoa, alisema yupo tayari kupoteza maisha ama kukosa kazi aliyokuwa nayo, kwani atahakikisha anakula sahani moja na watu wanaojihusisha na biashara hiyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment