Monday 26 September 2016

PROFESA ANNA TIBAIJUKA ASHINDA TUZO MAREKANI






Usiku wa September 24 2016 heshima nyingine ya Tanzania iliandikwa nchini Marekani baada ya aliyewahi kuwa Waziri wa Ardhi, nyumba na maendeleo ya makazi Profesa Anna Tibaijuka kushinda tuzo ya kimataifa ya ‘His Royal Highness Prince Khalifa bin Salman Al Khalifa Award  for Sustainable Development‘  ikiwa ni kutambua mchango wake katika kuhamasisha maendeleo duniani.

Tuzo hizi za heshima hutolewa kila baada ya miaka miwili ambapo washiriki wakuu huwa ni wale waliowahi kufanya kazi na shirika la umoja wa mataifa ambapo mwaka huu Waziri mkuu wa Bahrain Khalifa bin Salman ndiye aliyemkabidhi tuzo hiyo Profesa Tibaijuka.

Kazi ya utoaji wa tuzo hizi ulifanyika katika makao makuu ya umoja wa mataifa New York Marekani ambapo viongozi mbalimbali duniani walishiriki kushuhudia tukio hilo huku Tanzania ikisindikizwa na  Waziri wa mambo ya nje Balozi Augustine Mahiga pamoja na mbunge wa viti maalum Anna Lupembe.

No comments:

Post a Comment