Monday 12 June 2017

BREAKING NEWSSSSSS. MADINI YA TRILIONI 188.58 YAIBWA KWA MIAKA 17, MAWAZIRI WA ZAMANI WA MADINI, WANASHERIA WAKUU WAPO KIKAANGONI



Rais Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza baada ya kupokea ripoti ya pili ya Kamati ya Wachumi na Wanasheria aliyoiunda kwa ajili ya kuchunguza Mchanga wa Madini unaosafirishwa kwenda nje ya nchi, Ikulu jijini Dar es salaam leo. 

Katika ripoti hiyo iliyotolewa na Kamati imebaini kuwa Kampuni ya ACACIA MINE PLC haikusajiliwa nchini wala haina hati ya usajili na inafanya biashara ya madini nchini kinyume cha sheria.

Pia Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Profesa Nehemia Osoro alisema kuwa Serikali imepoteza Kodi ya Mapato ya kiasi cha sh. trilioni 55 tangu mwaka 1998 hadi Machi 2017 katika usafirishaji wa makinikia, bilioni 94 Kodi ya Zuio ambayo Tanzania imepoteza tangu 1998 hadi Machi 2017 na kufanya Jumla ya thamani ya madini yaliyosafirishwa nje ya nchi kati ya 1998 hadi 2017 kwa Kiwango cha wastani ni trilioni 188.58.

Rais Magufuli ameridhia mapendekezo ya kamati hiyo ya kutaka waliowahi kuwa mawaziri wa nishati na madini, wanasheria wakuu na watumishi wote wa serikali waliozembea ama kushiriki katika hujuma hiyo, kuchukuliwa hatua za kisheria.


No comments:

Post a Comment