Monday, 4 January 2016
12 WATIMULIWA KAZI KWA RUSHWA
Na Chibura Makorongo, Shinyanga
MAMLAKA ya Maji Safi na Mazingira katika Manispaa ya Shinyanga (SHUWASA), imewafukuza kazi watumishi 12, kutokana na vitendo vya rushwa na kuwabambikizia bili wateja wao.
Mkurugenzi wa mamlaka hiyo, Mhandisi Silvester Mahole, alisema hayo jana, ofisini kwake mjini hapa na kuongeza kuwa, hatua hiyo imechukuliwa kutokana na kuwepo kwa malalamiko kutoka kwa wateja.
Mhandisi Mahole alisema kutokana na hali hiyo, watumishi 12 wamefukuzwa kazi kwa makosa ya kujihusisha na vitendo vya rushwa.
Alisema watumishi hao wanapowakatia maji baadhi ya wateja waliochelewa kulipa bili, hupokea fedha na kwamba muda mwingine wanasoma mita kwa kukadiria.
Mhandisi Mahole alisema lengo la mamlaka hiyo ni kuboresha mtandao wa maji katika wilaya hiyo.
Alisema hadi sasa watu wanaonufaika na mtandao wa maji ni asilimia 60.6, ikiwa mfumo wa usambazaji upo katikati ya mji.
Mhandisi Mahole alisema manispaa hiyo inazo kata nne, ambazo hazina mtandao wa maji, ambazo ni Mwawaza, Chibe, Kolandoto na Ndala.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment