MHANDISI Ronald Lwakatare ameteuliwa
kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Mabasi Yaendayo Haraka Jijini Dar-es-
Salaam (DART).
Uteuzi huo umefanywa juzi na
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa
(TAMISEMI), George Simbachawene.
Akisoma taarifa hiyo kwa niaba ya
Simbachawene, Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano Serikalini , Ofisi ya Rais
TAMISEMI, Rebecca Kwandu, alisema uteuzi huo ulianza juzi.
Rebecca alisema Simbachawene
amefanya uteuzi huo kutokana na mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 2 (2)
cha amri ya kuanzisha wakala huo wa DART, tangazo la serikali namba
120 la mwaka 2007.
Alisema uteuzi huo unafuatia
kusimishwa kazi kwa aliyekuwa Mtendaji Mkuu, Asteria Mlambo,
aliyesimamishwa Desemba 23, mwaka jana.
Asteria alisimamishwa kazi ili
kupisha uchunguzi dhidi yake kutokana na tuhuma mbalimbali zinazomkabili
kuhusiana na wakala huo.
Rebecca alisema awali, Mhadisi
Ronald alikuwa Naibu Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Mfuko wa Barabara,
akishughulikia ufuatiliaji na tathmini.
Alisema mtendaji huo mpya anatakiwa
kuripoti kazini na kuanza kazi mara moja.
No comments:
Post a Comment