Monday, 30 May 2016
RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI MWINGINE
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa viongozi wengine wa tatu.
Rais Magufuli amemteua Jaji Shabani Ally Lila kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani.
Kabla ya uteuzi huo Jaji Shabani Lila alikuwa Jaji Kiongozi,Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.
Wakati huo huo, Rais Dkt. Magufuli amemteua Spika wa Bunge Mstaafu, Anne Semamba Makinda kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF).
Uteuzi wa Anne Semamba Makinda umeanza tarehe 25 Mei, 2016.
Anne Semamba Makinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Ali Mchumo.
Katika hatua nyingine, Rais Magufuli amemteua Prof. Apollinaria Elikana Pereka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Teknolojia Dar es salaam (Dar es salaam Institute of Technology - DIT).
Prof. Apollinaria Elikana Pereka ni Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Morogoro.
Prof. Pereka anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Prof. Fredrick Mwanuzi ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi huu umeanza leo tarehe 30 Mei, 2016.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment