Friday 23 September 2016

POLISI YARUHUSU MIKUTANO YA NDANI YA KISIASA


JESHI la Polisi nchini limeondoa katazo lake la mikutano ya ndani kwa vyama vya siasa kuanzia leo. 

Kamishna wa Oparesheni na Mafunzo wa Jeshi la Polisi, Nsato Mssanzya

ametangaza kuondoa zuio hilo leo na kusema kuwa makatazo mengine ya mikutano ya vyama hivyo yako pale pale.

 
Kamishna Mssanzya amesema mikutano ya hadhara na maandamano bado hairuhusiwi lakini wabunge wanaruhusiwa kufanya mikutano yao katika majimbo yao kwa mujibu wa katiba. 


Polisi imesema imeamua kuruhusu mikutano hiyo ya ndani baada ya kuridhishwa na mwenendo wa shughuli za kisiasa nchini.

No comments:

Post a Comment