Sunday 30 August 2015

MTATURU AITABIRIA KIFO CHADEMA




NA PETER KATULANDA, MWANZA

KATIBU wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) mkoani Mwanza, Miraji Mtaturu,
amewasihi wakazi wa Mwanza wasijaribishe mtu badala ya nguo.

Amesema CHADEMA ina mgombea urais mchovu na ilishindwa kuzindua kampeni kwa kuwa baada ya Katibu Mkuu wao, Dk. Willbroad Slaa kutimka waliobaki walishindwa kutayarisha ilani ya uchaguzi.

Katibu huyo alisema hayo kwa nyakati tofauti juzi kwenye mkutano wa hadhara wa kunadi wagombea ubunge na udiwani wa CCM.

Alisema siku zote mnafiki na muongo hawana kumbukumbu, CHADEMA na wenzao walisema CCM inakumbatia mafisadi na kumnyooshea kidole Lowassa, CCM ikasikia kilio cha Watanzania waliowakilishwa na vyama hivyo kikamtosa na kuchagua mwadilifu Dk. John Magufuli.

“Lakini kwa kuwa mnafiki na muongo hawana kumbukumbu,sasa wamempokea fisadi mkuu waliyeshinikiza ajiuzulu na kugeuza santuri na kanga hawaimbi tena ufisadi wanasema tatizo ni mfumo wa CCM,” alisema na kushangiliwa na umati wa wana Khang’anga Mkuyuni wilayani Nyamagana.

“Msijaribu mtu jaribuni mashine na magauni mkifanya hivyo mtajuta miaka mitano ijayo, Lwassa sasa kwa kujua mwisho wake umefika ndiyo maana anaanza kujifunza kupanda daladala na kula kwa mama ntiulie ili wasahau kama alipiga dili la Richmond.

Baada ya Katibu huyo kuwaombea kura Dk Magufuli, mgombea ubunge wa Nyamagana Stanslaus Mabula  na  mgombea udiwani Kata ya Mkuyuni, Donatha Gapi, wafuasi 12 wa CHADEMA , CUF na ACT Wazalendo wakiwemo walirudisha kadi za vyama vyao na kujiunga na CCM.

No comments:

Post a Comment