Na
Latifa Ganzel, Morogoro
ALIYEKUWA
Meneja wa Kampeni wa mgombea udiwani kupitia CHADEMA, Amos Chacha wa Kata ya
Mkundi, Jimbo la Morogoro Mjini, amejiunga na CCM.
Meneja kampeni
huyo, ambaye pia alikuwa katibu, alisema hayo jana, wakati wa uzinduzi wa
kampeni za mgombea udiwani wa kata hiyo, Hilda John, zilizofanyika kwenye kata
ya Mkundi, jimboni humo.
Chacha
alisema anajutia muda aliopoteza akiwa huko, ambako hakuna maendeleo yoyote
zaidi ya ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe, ambao hauna faida kwa chama.
Alisema
akiwa kijana aliyesomeshwa na serikali ya CCM tangu akiwa kidato cha kwanza
hadi chuo na kupata shahada ya juu ya sheria, hana sababu ya kukisaliti chama
hicho na kuendelea kubaki kwenye chama pinzani.
“Kuwafahamu
viongozi waliokuwa imara, kaa nao.
Nilikakaa
nao na ndipo nikatambua kuwa hawapo sawa, nikaamua kurudi, siwezi kumuuza Mwalimu
Nyerere na kwenda chama kisichoniwezesha kwa chochote,” alisema Chacha.
Akinadi sera
zake, mgombea udiwani wa kata hiyo, Hilda alisema akichaguliwa, atasogeza
huduma za kijamii ikiwemo maji, umeme, barabara, kusimamia ujenzi wa shule ya
msingi na sekondari ya kata sambamba na huduma za afya.
Alisema
ikiwa wananchi hao watamchagua, atahakikisha huduma hizo zinawafikia kwa wakati
ili kuondoa umaskini kwa jamii hiyo unaorudisha nyuma maendeleo ya watu.
“Mkinichagua
nitahakikisha tunapigana na maadui watatu wa maendeleo, ikiwemo umaskini,
ujinga na maradhi na kufanya kata yetu kusonga mbele kwa kuinua uchumi wa mtu
mmoja mmoja na vikundi mbalimbali kimikopo,” alisema.
Naye
Katibu Mwenezi wa CCM Wilaya ya Morogoro Mjini, Maulidi Chambilila, aliwaomba
wakazi wa kata hiyo kuwachangua viongozi wa CCM kwa kuzingatia mafiga matatu ya
urais, ubunge na udiwani ili kuifanya serikali na wananchi wake kuweza kupiga
hatua kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment