Friday 16 October 2015

MAGUFULI AFUNIKA UNGUJA








VIONGOZI wa Chama Cha Mapinduzi (CCM)  wamewataka wanaCCM kuendeleza amani na utulivu iliyopo hasa katika kipindi hichi cha kuelekea uchaguzi mkuu.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM uliofanyika katika viwanja vya MnaziMmoja, mjini Zanzibar  walisisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi alimuomba MwenyeziMungu kuufanya uchaguzi mkuu ujao uwe wa amani na salama.

Mzee Mwinyi aliwaomba wanaCCM kuhakikisha kuwa wanalinda amani na kutaka ibakie ili uchaguzi mkuu ujao uwe wa amani.

Alisisitiza kuwa ni lazima kufanyike juhudi za makusudi ili kupatikana ushindi na CCM itashinda kwani ina sifa na inastahiki kushinda huku akimuelezea Dk. Magufuli na Dk. Shein kuwa ni wachapa kazi.

CCM ni chama chenye maarifa na kinachojua mambo ila kuna watu wachache wanao haribu mambo na kusema kuwa tayari Dk. Magufuli ameshawapiga darubini kwani ana sifa za uongozi, mkweli, muadilifu, mpenda watu, muaminifu hana ubaguzi na akishinda atakuwa mwema kwa watu wote.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika mkutano wa Kampeni ya uchaguzi wa CCM uliohudhuriwa na maelfu ya wananchi na wanaCCM uliofanyika katika viwanja vya MnaziMmoja, mjini Zanzibar  walisisitiza amani kuelekea uchaguzi mkuu ujao.

Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ali Hassan Mwinyi alimuomba MwnyeziMungu kuufanya uchaguzi mkuu ujao uwe wa amani na salama.

Mzee Mwinyi aliwaomba wanaCCM kuhakikisha kuwa wanalinda amani na kutaka ibakie ili uchaguzi mkuu ujao uwe wa amani.

Alisisitiza kuwa ni lazima kufanyike juhudi za makusudi ili kupatikana ushindi na CCM itashinda kwani ina sifa na inastahiki kushinda huku akimuelezea Dk. Magufuli na Dk. Shein kuwa ni wachapa kazi.

CCM ni chama chenye maarifa na kinachojua mambo ila kuna watu wachache wanao haribu mambo na kusema kuwa tayari Dk. Magufuli ameshawapiga darubini kwani ana sifa za uongozi, mkweli, muadilifu, mpenda watu, muaminifu hana ubaguzi na akishinda atakuwa mwema kwa watu wote.


Aidha, alisisitiza kuwa kwa upande wa Zanzibar kura zote apewe Dk. Shein na kwa Tanzania nzima apewe Dk. Magufuli ili kuanza nchi mpya na kuuliza Zanzibar ya leo sawa na ya zamani.

Alisema kuwa Zanzibar imebadilika kutokana na maendeleo makubwa yaliopatikana katika sekta mbali mbali na kusisitiza kuwa kura zote wapewe viongozi wa CCM wanaogombania nafasi.

Nae Mjumbe wa Kamati Kuu ya Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Muhammed Kharib Bilal kwa upande wake alisema kuwa chama cha CUF kimekuwa na kauli za kuibiwa kila kipindi cha uchaguzi kinapofika na kueleza kuwa kauli hizo zinaonesha wazi kuwa chama hicho hakikubaliki.

Alisema kuwa Dk. Magufuli ni mchapa kazi, muadilifu, anakipenda chama chake, anapenda Muungano, hapokei rushwa, hajawahi kushughulikiwa kwa ufisadi hata mara moja.

Nae Makamu wa Pili wa Rais Balozi Seif Idd akiwasalimia wananchi alisema kuwa wapinzani wapende wasipende ushindi wa CCM ni jambo la lazima na kuwasisitiza wanaCCM wapambe maskani zao na matawi yao kwa ajili ya kusherehekea ushindi.

Alisema kuwa hivi sasa wapinzani wamekuwa wakisema maneno yaliopo na yasiopo huku akirejea kauli ya Maalim Seif alipokwenda Tume ya Uchaguzi kutaka kuapishwa eti akisema kuwa yeye tayari ameshashinda uchaguzi.

Balozi Seif alisema kuwa ni vyama vya siasa vimekubaliana kuendesha kampeni za kistaarabu hivyo kuna kila sababu ya kundesha kampeni hizo kistaarabu ili kuiweka Zanzibar iwe ya utulivu na amani.

Aidha, alilaani kitendo cha kuwekwa rangi nyekundu katika picha za kampeni za Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein katika maeneo ya Chukwani na kusema kitendo hicho ni cha kichokozi.

Alieleza kuwa Zanzibar haitaki vurugu na kama ameshaamua kuwaambiwa wafuasi wake wafanye vurugu CCM haiko tayari na hilo.

Aidha, aliwaonya wale wote walioamua kufanya vurugu siku ya uchaguzi mkuu vyombo vya dola havitokuwa tayari kuona hilo likitendeka.

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi Tanzania ambaye pia,  ni Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Alhaj Gulembo aliwataka Wazanzibari kutokuwa na wahaka kwani viongozi wote wa CCM wanaogombania nafasi watashinda na waliobaki ni kalagabao.

Akieleza kuhusu mabadiliko walieleza kuwa wanamnukuu vibaya Mwalimu kuhusu mabadiliko kuwa wakiyakosa ndani ya CCM watayapata nje ya CCM, hiyo ni kwamba CCM ikiendelea kuwaweka mafisadi ndani ya chama hicho ndio hilo linalotokea na kuuliza kati ya Magufuli na Lowasa nani fisadi.

Alisema kuwa kwa upande wa Zanzibar Maalim Seif Sharif ndio ni fisadi kwani alichokuwa akikitaka yeye ni ukubwa ili aweze kupata ulinzi na kueleza kuwa Ikulu ni sehemu ya pekee na wanaenda watu maalum.

Alisema kuwa Maalim Seif alikuwa na Lipumba na Lipumba baada ya kuondolewa kwenye dili la urais na kuingia Lowasa akaamua kuachia ngazi kwani hakuwa tayari kununuliwa.

Akimnadi Dk. Shein, Dk. Bilal alisema kuwa Dk. Shein ni mchapakazi, muaadilifu, anaependa watu anaetetea wananchi, anaependa chama chake na wanachama wake na anaetetea Muungano na Mapinduzi ya Januari 12, 1964.

Nae Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar alitoa pongezi kwa wanaCCM waliofurika katika mkutano huo na kusema kuwa umati mkubwa uliohudhuria katika mkutano huo ni ishara tosha kuwa Dk. Magufuli atachaguliwa kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Dk. Shein kuwa Rais wa Zanzibar.

Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Mjini, Borafya Ame Silima alieleza kuwa tayari CCM imeshapata ushindi na kilichobakia kwa viongozi hao ni kuapishwa akiwemo Dk. Shein kwa upande wa Zanzibar na Dk. John Magufuli kwa upande wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

No comments:

Post a Comment