Sunday 4 October 2015

MWENYEKITI WA DP MCHUNGAJI MTIKILA AFARIKI KWA AJALI


Mwanasiasa mkongwe nchini na Mwenyekiti wa Chama cha DP, Mchungaji Christopher Mtikila, amefariki dunia leo asubuhi.

Mchungaji Mtikila amefariki katika ajali ya gari iliyotokea katika kijiji cha Msolwa kilichoko Chalinze mkoani Pwani.

Kamanda wa Polisi mkoa wa Pwani, Jaffari Ibrahim amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo, iliyopoteza uhai wa Mchungaji Mtikila.

Alisema Mtikila alikuwa akitokea Morogoro kwenda Dar es Salaam na kwenye gari hilo kulikuwemo na watu wengine watatu, ambao wamejeruhiwa na kulazwa kwenye Hospitali ya Tumbi, Kibaha.

Alisema chanzo cha ajali hiyo hakijaweza kufahamika, lakini polisi wanaendelea na uchunguzi.

No comments:

Post a Comment