Wednesday 28 October 2015

BREAKING NEEEEWSSSSS....UCHAGUZI MKUU RAIS WA MUUNGANO HAUWEZI KUFUTWA-NEC


TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), imesema kufutwa kwa matokeo ya uchaguzi wa rais na wawakilishi visiwani Zanzibar, hakuwezi kuathiri mchakato wa uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani wa Jamhuri ya Muungano.

Mwenyekiti wa NEC, Jaji mstaafu Damian Lubuva, amesema jioni hii kuwa, uchaguzi wa rais na wabunge unasimamiwa na tume yake visiwani Zanzibar na kwamba ZEC haihusiki na mchakato huo.

Aidha, Lubuva alisema tayari NEC  imeshapokea matokeo ya kura za urais na ubunge kutoka majimbo yote ya Zanziba na hakukuwa na malalamiko yoyote yaliyowasilishwa kwake kulalamikia uchaguzi huo.

Mwenyekiti huyo wa NEC pia alisema mwaka 2005, NEC ilisimamisha uchaguzi mkuu wa Jamhuri ya Mungano baada ya mgombea mwenza wa urais wa CHADEMA kufariki dunia, lakini ZEC iliendelea na mchakato wake wa uchaguzi kama kawaida.

Amewataka wananchi kutosikiliza taarifa potofu na za uzushi zinazosambazwa na mitandao ya kijamii kwamba, NEC nayo imefuta matokeo ya uchaguzi kutokana na ZEC kufanya hivyo kule Zanzibar.

No comments:

Post a Comment