Friday, 5 February 2016

RAIS MAGUFULI ATOA MAELEKEZO KWA MAJAJI NA MAHAKIMU

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli akisisitiza jambo kuhusu utendaji wa Mahakama na Utoaji wa Haki kwa wananchi kwa wakati kwenye maadhimisho ya Siku ya Sheria. Mhe. Rais alikuwa mgeni rasmi kwenye maadhimisho hayo yaliyohudhuriwa na viongozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi.
Jaji Mkuu wa  Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman akiwahutubia viongozi, mabalozi na wageni mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.
Jaji Mkuu wa Kenya Dkt. Willy Mutunga (kulia) akimkabidhi zawadi ya kumbukumbu kutoka nchini Kenya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar es salaam. Jaji Mkuu wa Kenya alikua miongoni mwa wageni mashuhuri walioalikwa na Mahakama ya Tanzania kuhudhuria maadhimisho ya Siku ya Sheria.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka Mahakimu na Majaji wa Mahakama ya Tanzania kufanya kazi kwa kuzingatia weledi wa taaluma ya Sheria katika kushughulikia mashauri  yanayopelekwa Mahakamani.

Aidha amewataka Majaji na Mahakimu kutoa hukumu za mashauri  yanayowasilishwa Mahakamani kwa haraka ili kuwasidia wananchi wanaotafuta haki.


Akizungumza na mamia ya wageni kutoka ndani na nje ya nchi waliohudhuria Maadhimisho ya Siku ya sheria, Dkt. Magufuli amewataka Majaji na Mahakimu hao kutanguliza Uzalendo na maslahi ya taifa mbele pindi wanapotoa maamuzi ya mashauri yaliyoko Mahakamani.


 Mhe. Rais amemtaka Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Mohamed Chande Othman  kuchukua hatua kwa watendaji wa Mahakama wanaokiuka maadili kwa kufanya vitendo vinavyochafua taswira ya Mahakama mbele ya macho ya jamii.

Aidha, Katika hotuba yake Mhe. Rais amesema kuwa Serikali ya awamu ya tano itaendelea kuijengea uwezo wa kifedha Mahakama ili iweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.

No comments:

Post a Comment