JESHI la Polisi limewatoa hofu wananchi kuhusiana na kuonekana kwa baadhi ya askari wakifanya mazoezi katika maeneo mbalimbali nchini.
Taarifa iliyotolewa jana na jeshi hilo, ilisema katika siku za hivi karibuni, kumekuwepo na mitazamo tofauti miongoni mwa jamii kufuatia kuonekana kwa askari polisi wakifanya mazoezi.
"Kufuatia hali hiyo, jeshi la polisi nchini linatumia fursa hii kuwatoa hofu wananchi kwamba, mazoezi hayo ni ya kawaida kwa askari wa jeshi la polisi," ilisema taarifa ya jeshi hilo.
Pia, limewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za kawaida kwa sababu mazoezi hayo hayalengi kuzuia shughuli zozote halali zinazofanywa na wananchi.
No comments:
Post a Comment