Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini |
Umati wa wananchi ukimsikiliza Mgombea Mwenza kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu alipohutubia mkutano wa kampeni katika eneo la Msange, Singida Kaskazini |
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akiwasalimiabaadhi ya viongozi, baada ya kuwasili katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika jimbo hilo. |
Mgombea Mwenza wa Urais kwa tiketi ya CCM, Mama Samia Suluhu Hassan akimnadi Mgombea Ubunge Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandu, katika mkutano uliofanyika katika jimbo hilo |
Mgombea Ubunge wa Iramba Magharibi, Mwigulu Nchemba akiselebuka na baadhi ya viongozi na wananchi katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, katika eneo la Kyengege, Iramba mkoani Singida, |
NA EPSON LUHWAGO, SINGIDA
HOSPITALI kubwa ya
kisasa inatarajiwa kujengwa mkoani hapa, ambayo itakuwa ya rufani kwa mkoa wa Singida
na mikoa inayouzunguka, imeelezwa.
Hayo yalisemwa jana na
Mgombea Mwenza wa Urais wa CCM, Samia Suluhu Hassan, alipokuwa katika
mikutano ya kampeni ya Chama Singida
Mjini na Kyengeja, wilayani Iramba.
Samia alisema hospitali
hiyo itakuwa kubwa na ya kisasa na itahudumia wagonjwa kutoka mikoa ya Singida,
Dodoma, Tabora, Simiyu na Manyara.
“Hospitali hii itakuwa ya
rufani kama ile ya Muhimbili (Dar es Salaam) na itapunguza adha ya kufuata
huduma Dar es Salaam au Mwanza. Kukamilika kwa hospitali hii kutawezesha huduma
bora za afya kupatikana kwa urahisi,”alisema.
Sambamba na hospitali
hiyo, alisema huduma za afya zitaboreshwa zaidi kwa kuongeza wataalamu na vifaa
tiba.
Mbali na huduma za afya,
alisema mkazo mkubwa mwingine utakuwa katika ujenzi wa viwanda vya kusindika
mazao na kuchakata madini ili viweze kutoa ajira kwa vijana na wananchi wa mkoa
wa Singida.
Miongoni mwa viwanda
hivyo, kwa mujibu wa Samia, ni vya kusindika mafuta ya alizeti kutokana na mkoa
huo kuzalisha zao hilo kwa wingi kulinganisha na mikoa mingine.
Alisema kwa sasa kuna
viwanda vidogo vya kutengeneza mafuta hayo lakini kuna kiwanda kikubwa ambacho
kinajengwa katika eneo la Ndago.
Samia alisema kukamilika
kwa kiwanda hicho kutawezesha kutoa ajira zaidi kwa vijana hivyo kupunguza
tatizo hilo ambalo ni kubwa nchini kote.
“Kiwanda hiki kikikamilika
kitachuja mafuta kwa mara ya pili (double refinery) ambayo yatakuwa na ubora wa
hali ya juu yatakayoweza kuuzwa katika masoko ya kimataifa,” alisema.
Samia alisisitiza kuwa kukamilika
kwa kiwanda hicho na vingine ambavyo viko mkoani Singida vitaweza kuajiri zaidi
ya vijana 600.
Mgombea mwenza huyo
alisema serikali ijayo ya CCM itahakikisha inasambaza umeme kwa kasi zaidi
kwenye vijiji.
Kwa mujibu wa Samia, umeme
huo utachochea ukuaji wa uchumi kwa kuwa wananchi wataweza kuanzisha viwanda
vidogo vya kutengeneza vitu mbalimbali.
Katika mkutano wake wa
kwanza mkoani Singida katika kijiji cha Msange, Jimbo la Singida Kaskazini,
alisema tatizo la maji ambalo linavikabili vijiji vingine vya Singida,
litapatiwa ufumbuzi katika serikali ijayo ya awamu ya tano chini ya CCM.
Pia alisema elimu alisema
jitihada kubwa zitakuwa ujenzi wa mabweni na kukamilisha maabara ili kuwezesha
watoto wengi hususan wa kike, kutoendelea kukatisha masomo kutokana na mimba.
“Kujengwa kwa mabweni
haya, kutawezesha watoto wengi kukaa shuleni kwani watakuwa katika mazingira
rafiki tofauti na sasa ambapo wanatembea umbali mrefu kuwenda shuleni na kurudi
nyumbani,” alisema.
NYALANDU NA HELIKOPTA
Mgombea Ubunge katika
Jimbo la Singida Kaskazini, Lazaro Nyalandi, jana aliteka hisia wa wananchi
waliokuwa kwenye mikutano ya kampeni za CCM pale alipotua kwa helikopta.
Nyalandu ambaye anagombea
kwa mara ya nne katika jimbo hilo, aliwasili kwa ‘chopa’ hiyo saa 4.57 katika
kijiji cha Msange ambapo baada ya kutua mkutano ulilipuka furaha huku Katibu
Mkuu wa UWT, Amina Makilagi, akihanikiza kuwa ‘jembe linaingia’.
Mbunge huyo ambaye pia ni
Waziri wa Maliasili na Utalii, alitua kwa usafiri huo katika mikutano
iliyofanyika Kyengege jimbo la Iramba na Singinda Mjini ambako mkutano mkubwa
ulifanyika kwenye viwanja vya CCM Mkoa.
Kutumika kwa usafiri huo
na kiongozi huyo, kulikuwa kinogesho cha aina yake kwa kuwa alikuwa akitua baada
ya watu kukusanyika na wakati mwingine kuanza kwa shughuli za kampeni sehemu
husika.
MWIGULU ATOA NENO
Naye Mwigulu Nchemba,
anayetetea kiti cha ubunge Jimbo la Iramba, alisema mambo ambayo CCM imeyafanya
katika mikoa wa Singida, ni mtaji tosha kwa Chama kushinda tena kwa nafasi ya
urais, ubunge na udiwani.
Alisema CCM imefanya mambo
makubwa kwa kujenga shule za sekondari katika kila kata na kuboresha huduma za
afya kuanzia ngazi za vijiji kwa kujenga zahanati.
Kwa mujibu wa Mwigulu,
hata ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ni ishara tosha kuwa CCM inataka
kurejea ili kuwaleta wananchi maendeleo zaidi.
“Hivi sasa katika jimbo la
Iramba kwa mfano, kuna umeme katika vijiji vingine na kazi ya kupeleka kule ambako
haujafika inaendelea.
Tunahitaji kuichagua tena
CCM ili kumalizia kazi hii,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Yule
ambaye atawapigia wapinzani atakuwa anapoteza muda na nguvu zake. CCM itashinda
na kuendelea kushika dola. Wapinzani hao hawana uwezo kwasababu ni waigizaji na
kuishindanisha CCM na waigizaji ni jambo ambalo haliwezekani.”
Mwigulu, ambaye ni Naibu
Waziri wa Fedha, aliwataka wananchi waliojitokeza kwa wingi kupiga kura Oktoba
25, mwaka huu, ili waichague CCM na kuipa ushindi wa kishindo.
No comments:
Post a Comment