Sunday, 11 October 2015

LOWASSA AWAPIGIA DEBE WAGOMBEA WA CCM




MGOMBEA urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, amewataka wananchi wa Sirari mkoani Mara, kuwachagua wagombea wa Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Lowassa, ambaye alikuwa akihutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika katika viwanja vya Tarafa katika Mji Mdogo wa Sirari, aliwaomba wananchi kuwachagua wagombea ubunge na madiwani kutoka CCM na kwa upande wa urais apewe yeye.
Huku akionekana kuwa na uchovu pamoja na kuendeleza staili yake ya kuhutubia chini ya dakika sita, Lowassa alihutubia mkutano huo ambao ulijaza idadi kubwa ya watu kutoka nchi jirani ya Kenya, ambao walivuka mpaka.
''Nawaomba wananchi wote mliofika hapa kuwa kura zote za udiwani na ubunge muwape wagombea wote wa CCM, halafu za urais mnipe mimi zote bila kujali itikadi ili niweze kuleta maendeleo hasa upande wa elimu kama kipaumbele changu,'' alisema.

Kauli hiyo ya Lowassa iliibua minong’ono kutoka kwa wafuasi wa CHADEMA, ambao walionekana kushangazwa huku wengine wakijaribu kuhoji uimara wa mgombea huyo.

No comments:

Post a Comment