NA SHAABAN MDOE, ARUSHA
KATIBU Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, amesema aliyekuwa mgombea urais wa CHADEMA, Edward Lowassa, alishindwa kuhutubia kwa zaidi ya dakika tatu, hivyo hakuwa na lolote la kumkariri.
Kinana alitoa majibu hayo baada ya Lowassa kudai kuwa kazi nzuri anazozifanya Rais Dk. John Pombe Magufuli ni utekelezaji wa sera za vyama vinavyounda UKAWA.
Alisema mgombea huyo hakuwa na hotuba yoyote kwa kuwa hakuweza kuongea hata kwa zaidi ya dakika tatu katika mikutano yake aliyoifanya.
Pia, alimshangaa Lowassa kuwa mbali na kushindwa kuzungumza, hakuwa na hotuba yoyote ambayo ingeweza kukaririwa na Dk. Magufuli na hakuweza kuzungumzia masuala yoyote ya kupambana na

ufisadi kwa kuwa yeye ndiye kubwa la mafisadi na vyama vinavyounda UKAWA ndiyo vimeukumbatia
ufisadi kwa sasa.
Kinana aliyasema hayo jana alipokuwa akihutubia mkutano wa hadhara wa kampeni za mgombea ubunge wa jimbo la Arusha, Phillemon Mollel (Monaban) uliofanyika Kata ya Daraja Mbili.
Alisema sera ya kupambana na ufisadi ilizungumzwa katika kampeni na Dk. Magufuli peke yake na si Lowassa wala kiongozi yeyote anayetokana na UKAWA.
Aliongeza kuwa Lowassa alinadi sana mabadiliko iwapo angeweza kuingia madarakani, lakini hakufafanua ni mabadiliko yapi ambayo angeweza kuyaleta wakati anatoka katika mfumo uleule aliokulia kwa zaidi ya miaka 40 akiwa ndani ya CCM na serikali yake.
“Jamani alisema mabadiliko, lakini hao wanaotaka mabadiliko wana umri wa ujana sawa na jua linalochomoza la saa mbili asubuhi wakati anayedai kuleta mabadiliko ana umri wa uzee sawa na jua linalozama la saa 12.30 jioni si vichekesho hivyo,”alisema Kinana.
Alisema kutokana na ukweli huo ndiyo maana Watanzania walipima na kuamua kumpa ushindi wa kishindo Dk.Magufuli kutokana na uadilifu wake na uwezo wake wa kuchapa kazi na kuamua kumnyima Lowassa ambaye kwa sasa anajifariji kwa kusema sera zinazotekelezwa ni za UKAWA.
Akizungumzia kazi alizoanza kuzifanya Rais Magufuli, alisema zimewakuna Watanzania wengi na kuwa hiyo ndiyo kazi aliyoahidi kwao kuifanya na kwamba anaamini ataifanya kwa dhati katika kuwapiganiawananchi wanyonge.
Kinana alipingana na dhana inayoelezwa kuwa hakuna kiongozi yeyote atakayetokana na CCM anayeweza kupambana na machafu ndani ya serikali kwa kuwa hilo ni suala la mfumo.
Akieleza kuhusu dhana hiyo, alisema mfumo unaweza kubadilishwa hata na mtu mmoja kama anavyofanya Dk. Magufuli, Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.
Alisema moja ya mambo aliyoyaondoa katika mfumo huo ni kufuta safari za nje kwa viongozi akiwemo yeye binafsi, kuondoa semina, warsha, makongamano, sherehe, maadhimisho, posho na kuagiza fedha hizo kwenda katika mahitaji mengine ikiwemo hospitalini.
Alitolea mfano wa kufutwa kwa mambo hayo machache kuwa tayari Dk. Magufuli ameokoa zaidi ya sh. trilioni moja mbali na fedha zingine alizokusanya kutokana na kuwabana wakwepa kodi aliowabaini na kukutana nao na kuwapa muda kulipa kodi hizo.
Alisema hadi sasa, Dk, Magufuli amekataa safari tani za nje alikoalikwa ikiwemo Kenya, Afrika Kusini na Rwanda ambapo alizikataa na kusema iwapo zina umuhimu sana mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi hizo watashiriki.
Jingine alisema kuna mialiko aliyokataa kwenda kwenye baadhi ya nchi kwa ajili ya kufahamiana na viongozi wa mataifa makubwa akiwemo Malkia wa Uingereza.
Katika mwaliko huo, alisema Dk. Magufuli aliwaambia kama wanahitaji kujuana naye waje wao Tanzania, lakini si yeye kuwafuata.
Akizungumzia uchaguzi wa kesho, aliwataka wananchi wa jimbo la Arusha kuachana na ushabiki wa vyama na badala yake wachague kiongozi kutokana na sifa zake na kuangalia maslahi yao na si ya chama wala kiongozi husika.
Kinana alisema kwa sasa wananchi wa jimbo la Arusha wanapaswa kuangalia maslahi yao katika kumchagua mbunge yakiwemo maslahi ya shule, afya, miundombinu, amani na mambo mengine muhimu badala ya kubaki kuimbiwa kuwa wanafundishwa kuiwajibisha serikali huku wakibaki katika lindi la umasikini na ukosefu wa amani kutokana na kuwepo kwa maandamano kila kukicha.

No comments:
Post a Comment