MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akimkabidhi Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni ya Geita Gold Mining (GGM), Terry Mulpeter, tuzo ya maalumu ya kutambua mchango wa kampuni hiyo katika kujitoa kwake kuisaidia jamii ya watu wa Geita. Hafla hiyo ilifanyika juzi mkoani Geita.
MAKAMU
wa Rais, Samia Suluhu Hassan, amezindua miradi ya maendeleo katika mkoa wa
Geita, iliyofadhiliwa na mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) kwa ushirikiano na
serikali ya Tanzania.
Samia,
alizindua miradi hiyo jana, ambapo alianza kuzindua mradi mkubwa wa maji wenye
thamani ya sh. bilioni 12, uliojengwa kwa ushirikiano kati ya mgodi na serikali,
ambao utapunguza tatizo la maji safi na salama kwa mkoa huo kwa zaidi ya
asilimia 35.
Alisema
tatizo la maji lilikuwa kero kwa wakazi wa Geita kwa miaka mingi, ambapo kinamama
na watoto walikuwa wakitembea umbali mrefu ili kupata maji safi kwa matumizi ya
nyumbani.
Samia
alisema serikali imekusudia kuleta maendeleo ya kasi kwa wananchi kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo kama inavyodhihirika katika mradi
huo.
Aidha,
Samia alitembelea na kuzindua muendelezo wa Hospitali ya Rufani ya mkoa wa
Geita, ambayo ilijengwa mwaka 1957.
Miradi
mingine aliyoweza kuitembelea na kuizindua ni wa ushonaji na kudarizi, ulio
chini ya mradi mkubwa wa kuendeleza uchumi kwa wananchi wa Geita, uitwao Geita
Economic Development Program (GEDP), ambao unahusisha miradi ya kilimo cha
mpunga na alizeti, kufyatua matofali ya ‘interlocking blocks’ na uchomeleaji
utakaoweza kuleta ajira zaidi ya 300 kwa vijana wa mkoa wa Geita.
No comments:
Post a Comment