UMOJA
wa Vijana wa CCM (UVCCM), Wilaya ya Iringa Vijijini, umewasimamisha uanachama, wanachama
wake wawili kwa tuhuma za usaliti wakati wa uchuguzi mkuu wa mwaka 2015, ambao
ulimpa ushindi Dk. John Magufuli.
Akizungumza
na waandishi wa habari jana, wakati wa kikao cha tathmini ya uchaguzi huo, Mwenyekiti
wa UVCCM wilayani hapa, Benitho Kayugwa, alisema wametoa maazimio hayo baada ya
kubaini makada hao kuwasaliti.
Alisema
baada ya kufuata kanuni na taratibu za UVCCM, wameamua kuchukua uamuzi huo na
uchunguzi zaidi bado unaendelea kuwabaini wengine.
Aliwataja
waliosimamishwa uongozi na Kamati ya Utekelezaji ya UVCCM kuwa ni Mwenyekiti wa
Kata ya Mgama, Aidan Kising’a na aliyekuwa Katibu wa Kata ya Luhota, Maria Kibuga.
“Kamati
ya Utekekezaji ya UVCCM Wilaya ya Iringa Vijijini, imewasimamisha uongozi makada
wake wawili kwa tuhuma za kukisaliti chama,” alisema.
Naye
Katibu wa CCM Wilaya ya Iringa Vijijini, Dodo Sambu, alisema hatua waliyofikia
ya kuwavua uongozi wanachama waliokisaliti chama ni nzuri na kwamba kazi ya
kuwatumbua majipu wasaliti ni endelevu.
No comments:
Post a Comment