Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akiwasili kwenye uwanja wa Jamhuri tayari kuhutubia wakazi wa Morogoro mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM |
Wananchi wakimkaribisha Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli kwenye uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. |
Wanachama wa Chama Cha Mapinduzi wakifurahia ujio wa mgombea wa Urais wa CCM Dk.John Pombe Magufuli. |
NA
SELINA WILSON, MIKUMI
MAFISADI
wachache wanaomiliki fedha nyingi wanatajwa kuwa ndio chanzo kilichoifikisha nchi
kwenye umasikini na kwamba, wameanza kudhibitiwa ili kukomesha kabisa vitendo
hivyo.
Mgombea
urais wa CCM, Dk. John Magufuli, alisema hayo jana wakati akihutubia wananchi
wa Kijiji cha Ruaha katika Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, wakati wa ziara
yake ya kampeni za uchaguzi mkoani humo.
Dk.
Magufuli alisema kuna watu wachache wenye hela nyingi wakati kuna
Watanzania wengi hawana hela hivyo akipata ridhaa ya wananchi atasimamia na
kuhakikisha fedha zinashuka kwenda kwa wananchi.
Alisema
mafisadi wamekuwa wakitumia fedha zao hovyo na kwamba hata kwenye mchakato wa
uchaguzi mkuu wametumia mabilioni kununua mabasi na kufanya kila jitihada ili
wachaguliwe.
“Siwezi
kuacha hali hii iendelee. Mtu mmoja ananunua mabasi 30 kwa ajili ya uchaguzi
mkuu. Nipeni urais ili nikawashughulikie. Jina langu Magufuli, nipeni kura
nikawafunge magufuli yangu ili nikomeshe ufisadi,” alisema.
Alisema
kiu ya Watanzania walio wengi ni kutaka mabadiliko, lakini alionya wasikubali
mabadiliko ya jazba na badala yake washirikiane naye kuleta mabadiliko bora.
CHADEMA MBWA MWITU
Katika
hatua nyingine, Dk. Magufuli akiwa katika maeneo ya Mkamba na Ruaha aliwaponda
CHADEMA na kuwafananisha na mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo.
“Mchungaji
unachunga kondoo, ghafla akatokea mbwa mwitu naye akajiunga na kundi la
kondoo na kukawa hakuna tofauti, kondoo wapo wanaendelea na mambo yao kama
hakuna kilichotokea.
“Kwa
mchungaji ukiona kondoo hawashituki, ujuea uliokuwa ukiwachunga hawakuwa kondoo
bali ni mbwa mwitu waliojivika ngozi ya kondoo na ndio maana hawashangai kwa
kuwa yule mbwa mwitu ni mwenzao,” alisema.
Alisema
CHADEMA wamekuwa wakipiga vita ufisadi kila uchao na kuisema CCM kwamba
inakumbatia mafisadi sasa CCM imewaondoa wao ndio wamewakumbatia na kumteua
mmoja wao kuwa mgombea wao wa urais.
Dk.
Magufuli alisema kwa kitendo hicho CHADEMA ni mafisadi na wanakumbatia mafisadi
hivyo wananchi wasiwapigie kura na badala yake waichague CCM ili ilete
mabadiliko bora.
Aliwataka
wananchi kumpa rungu la kuwashughulikia mafisadi na kutoa mfano wa kitanda
kikiwa na kunguni unatakiwa kuwua kunguni ikibidi wachomwe kwa maji ya moto na
kitanda kiendelee kutumika.
Mapema
akizungumza kabla ya kumkaribisha Dk. Magufuli kuzungumza na wananchi, Mjumbe
wa Kamati Kuu na Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi, Abdallah Bulembo, alisema CCM
makada wake haikumteua Edward Lowassa wala Fredrick Sumaye kwa sababu ya
kashfa za ufisadi.
Alisema
CCM imeleta kada makini ,Mwanasayansi Dk. Magufuli ambaye ni mwiba kwa wapiga
dili na ndio maana walivyoona hivyo wakakimbilia UKAWA
KERO YA WAKULIMA WA MIWA
Wakati
huo huo nyingine Dk. Magufuli alisema anatambua kero kubwa ya uhusiano mbaya
kati ya wakulima wadogo, wakubwa na wenye viwanda vya sukari.
Alisema
akiwa Rais atashughulikia kero hiyo ili wakulima wapate haki yao badala ya
kudhulumiwa na walanguzi wanaotaka kunufaika huku wakulima wakishindwa
“Nimesikia
kuna NGO’S zinadhulumu wakulima wa miwa. Ushirika unawanufaisha wa watu wa juu.
Kwenye serikali ya Magufuli tutazimaliza kero hizo kwa kuwa tunataka watu
wanufaike na kazi wanazofanya,” alisema.
BEI YA SUKARI KUSHUSHWA
Akizungumzia
kuhusu bei ya sukari, alisema akiingia Ikulu atasimamia bei ya sukari ishuke
hususan kwa eneo la Ruaha, ambapo ndipo kiwanda kilipo kwa kuwa hakuna wananchi
wauziwe bei juu.
“Haiwezekani
kiwanda kipo hapa halafu bei ya sukari iwe sawa na Dar es Salaam. Kwa nini
isiuzwe kwa bei ya kiwandani. Niacheni hilo nitalimaliza,” alisema Dk. Magufuli
huku umati wa wananchi ukimshangilia.
Dk.
Magufuli alisema hakuna sababu sukari iende Dar es Salaam halafu ndio irudi kwa
wananchi na kuuzwa kwa bei ya juu, lazima wananchi wanufaike na uwepo wa
kiwanda.
Hatua
hiyo ya Dk. Magufuli kuzungumzia kero hiyo ilitokana na malalamiko ya wananchi
kwamba wanauziwa sukari kwa bei juu ya sh. 2,000 ambalo ndio kuna kiwanda cha
sukari cha Ilovo.
Juzi
akizungumza Mjini Ifakara, Mgombea ubunge jimbo la Kilombero, Aboubakar Asenga,
alimuomba Dk. Magufuli akiingia madarakani ashughulikie kero ya bei ya sukari.
No comments:
Post a Comment