Friday 11 September 2015

WOSIA WA BABA WA TAIFA KUHUSU UONGOZI


'Wapo viongozi wakishindwa kupata sifa, kupata kura kwa sera, kwa kusimama, ...wananchi tuchagueni kwa sababu mkishatuchagua, sisi tutafanya mambo kadha kadha... na wananchi wakawasikiliza vizuri na kwa makini wakaona naam, hawa wanafaa. Wanaposhindwa hivyo, wanatumia njia mbalimbali na moja inaweza ikawa ukabila na nyingine inaweza ikawa dini. Wanaweza wakajaribu kupata kura kwa kutumia ukabila au wakatafura kura kwa kutumia dini. Sasa kutafuta uongozi kwa kutumia dini au kwa kutumia kabila, unagawa watu. Kazi ya uongozi ni kujenga watu wawe kitu kimoja.  Kazi ya uongozi haiwezi kuwa ni kuwatenga watu waliokuwa na umoja wawe mbalimbali, si kazi ya uongozi, na hasa mahala ambapo bado hamjakomaa, bado mpo kwenye jitihada za kujenga. Wakianza viongozi wa namna hiyo na tukawakubalia, tutagawanyika.'

BABA WA TAIFA MWALIMU JULIUS KAMBARAGE NYERERE

No comments:

Post a Comment