Friday, 11 September 2015
WALINZI WA CHADEMA WAMPA KIPIGO MWANDISHI WA UHURU, WAMFUNGIA OFISINI KINONDONI, WAMSHIKISHA KADI ZA CHADEMA NA KUMPIGA PICHA
Chadema hizi ni siasa uchwara
Nimesikitishwa sana na kitendo walichofanya Chadema mapema leo kwenye ofisi zao mtaa wa Ufipa Kinondoni, jijini Dar es Salaam.
Mpiga picha wa gazeti la Uhuru Christopher Lissa baada ya kupata tetesi kwamba kuna wanachama wa chama hicho wanatarajia kuandamana kupinga kauli ya udini iliyotolewa na Lowassa, naye akaenda kusubiri tukio hilo kama waandishi wa habari wengine.
Chakushangaza, walinzi wanaolinda ofisi hizo walimfukuza kuwepo eneo hilo kwasababu anatoka kwenye gazeti la CCM, baadae wakaamua kumkamata kwa nguvu na kumuingiza kwenye moja ya ofisi zao wakampiga na kumbambikia kadi feki za Chadema wakadai amekamatwa nazo na haijulikani wanataka kutengeneza mazingira gani.
Tukio hili linafuata ikiwa ni siku chache baada ya mwandishi huyo kuandika makala inayoelezwa kuwakera mno Chadema na kuanza kumfuatilia na leo alipokwenda kwenye lao ikawa wamepata sababu.
Hizi ni dalili za kushindwa. Ni siasa uchwara ambazo zinapaswa kukemewa, kama wameanza mambo haya ya kubagua waandishi wa habari wakati hawajaingia ikulu, wakipata dola itakuaje? Uhuru wa habari utakuwepo?Msitupeleke huko
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment