Sunday, 4 October 2015

VIONGOZI WA CCM WATOA WOSIA KWA WANANCHI


Balozi Amina Salum Ali akimwaga sera za CCM
Baadhi ya viongozi wa CCM waliohudhuria mkutano huo
Wanachama wa CCM wakifurahia jambo wakati wa mkutano huo
Balozi Ali Karume akisisitiza jambo wakati wa mkutano huo

VIONGOZI wa CCM Zanzibar wamewataka wananchi na wanaCCM wa kisiwa cha Pemba kuepuka siasa za chuki zilizoanza kurejeshwa tena na wafusi wa chama cha CUF licha ya kuwa tayari chama hicho kimefanya maridhianao na hivi sasa kimo katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar yenye muundo wa Umoja wa Kitaifa.

Hayo waliyasema viongozi wa CCM Zanzibar katika Mkutano wa CCM wa Kampeni za uchaguzi uliofanyika huko Kiungoni, Jimbo la Mgogoni Mkoa wa Kaskazini Pemba uliohudhuriwa na maelfu ya wanaCCM.

Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Vuai Ali Vuai Na kusema kuwa CUF kuacha kufanya fujo na vurugu kwani vyama vimesema vitafanya Kampeni kwa amani na utulivu lakini CUF wameanza kuvunja taratibu hizo huku akisema kuwa Dk. Shein ametekeleza Ilani kwa zaidi ya asilimia 90 huku akisisitiza kuwa katika suala zima la ajira mipango kabambe imewekwa na Dk. Shein.

Akiwatambulisha kwa niaba wanachama wa CUF waliojiunga na CCM wakiwemo Bwana Rashid Mohammed Hassan ameamua kukihama chama cha CUF Khamis Halfan Khamis pamoja na wenzao kutoka Wete pamoja na Micheweni.

"uchaguzi wa mwaka huu CUF itapata kipigo cha paka mwizi kutokana na ushindi mkubwa utakaopatikana na  CCM"alisema Vuai.

Vuai aliwatambulisha wanachama wapya zaidi ya 40 ambao wamejiunga na CCM wakitokea CUF na kueleza kuwa CCM inaposema itapata ushindi wa asilimia 60 haitanii kwani imefanya maandalizi na vijana wamekuwa wakiiunga mkono chama hicho kwani wameshautambua ukweli uko wapi.


Vijana hao waliokihama chama cha CUF walitoa shukurani kwa CCM kwa kuwapokea na kumuhakikishia Dk. Shein kuwa kura zao zote zitaenda kwa wagombea wa CCM.

Walisema kuwa hivi sasa vijana wameamka na wamechoka kudanganywa kwani hakuna nchi duniani inayotoa ajira kwa vijana wote wakati mmoja na kusema kuwa wao wanahitaji kiongozi ambaye atatekeleza Ilani.


Walieleza kushangazwa na mgombea urais wa CUF anaepita kubadilisha maneno na kuwadanganya wananchi kwa kila anapohutubia mikutano yake ya kampeni na kumpongeza Dk. Shein kwa kutekeleza Ilani pamoja na kuishukuru CCM kwa kumsimamisha John Magufuli.

"Vijana wanahitajai serikali ambayo itakuwa na Ilani ya kuleta maendeleo, na na sio sera za CUF zinazozungumzia bajeti ya kununulia Pempas"walisema.

Nae Rashid alitoa shukurani kwa mapokezi makubwa aliyoyapata tokea, Mkoa, Wilaya hadi Wadi kwa lengo la kujiunga na CCM na kusema kuwa kilichomtoa katika chama cha CUF ni uongo mwingi.

Aidha, anasema CUF walimkataa kwa sababu alikuwa anashirikiana na CCM na anasema hivi sasa hana cha kufanya kwani mashamba na vitu vyake vyote vimeharibiwa na wafuasi wa CUF kwa madai kwamba yeye ni CCM.

Nae Bwana Khamis amesema kuwa ana furaha kubwa kwa kufika katika mkutano huo wa CCM na kuwaombea dua viongozi na wanaCCM wote huku akitoa shukurani kwa mapokezi makubwa aliyoyapata na kusema kuwa CCM anaipenda na imo moyoni mwake.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Kaskazini Pemba Mberwa Hamad Mberwa alisema kuwa bado wapo wafuasi wa vyama vya upinzani ambao bado wanaendesha siasa za chuki kisiwani humo ambao wamekuwa wakiwanyima wananchi bidhaa kwa sababu ya itikadi za kichama.

Alieleza kusikitishwa kwake na hujuma alizofanyika Bwana Rashid Mohammed baada ya Shamba lake la muhogo kulishwa ngombe usiku na kuharibu mazao yake yote ya muhogo kwa makusudi pamoja na kutiwa moto miti yake zaidi ya shamba kwa madai kuwa anawaunga mkono viongozi wa CCM.

Nae Bi Mauwa Daftari alisema kuwa mafanikio makubwa katika sekta za maendeleo yamepatikana katika Mkoa huo wa Kaskazini likiwemo Jimbo hilo la Kojani ikiwa ni pamoja na ujenzi wa miundombinu ya barabara katika Mkoa huo wa Kaskazini Pemba, huduma za afya, maji, umeme na nyenginezo.

Alisema kuwa Dk. Shein na John Pombe Magufuli ni watekelezaji na waadilifu na wala si viongozi vigeugeu kwani wanasema yale wanayoyaamini pamoja na yale yanayotekelezeka.

Nae Balozi Ali Karume alitumia fursa hiyo kuwaombea kura viongozi wote wa CCM wakiwemo mgombea Urais wa Zanzibar pamoja na wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kueleza kuwa Zanzibar imejijengea sifa kubwa duniani kwa kuwa na amani na utulivu.

"Balozi alikuwa anafanya kazi katika ubalozi wa Eletria alinieleza kuwa Zanzibar ina bahati kubwa sana kwa kuwa na amani na utulivu lakini hiyo inatokana na kuwa na kiongozi mzuri anaeiongoza Zanzibar"alisema Balozi Karume.

Aliwataka Wazanzibari kutodanganywa kwa kuvunja Muungano na kuona kuwa Muungano ni tatizo na kusema kuwa Zanzibar imekuwa ikisifika kutokana na amani na utulivu uliopo na kushangwaza na wale wanaoupinga Muungano.

Balozi Karume alishangazwa na maneno yanayosemwa na kiongozi wa CUF ya kuigeuza Zanzibar kuwa Singapore ambapo alisema kuwa kila nchi duniani itaendelea kwa juhudi zake wenyewe kwani kila ndege anaruka kwa ubawa wake na kusisistiza maneno ya mzee Karume kuwa mtu anatakiwa asifu chake na mpaka asahau cha mwenzake.

Balozi Amina Salum Ali alisema kuwa uchaguzi wa mwaka huu ni uchaguzi muhimu kwa Zanzibar na Tanzania nzima kwa jumla na kueleza kuwa  CCM imejijengea utaratibu mzuri wa kubadilisha wagombea wa urais kwa taratibu na Katiba yao ilivyoweka lakini CUF haina utaratibu huo.

Alisema kuwa CCM imejipanga vyema na kugusia kuwa huwezi kudai Mamlaka kamili wakati tayari Mamlaka Kamili yapo na wanaodai mamlaka hayo hawaelewi wanachokidai.

Alisema kuwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa imekuja kwa kutaka amani na utulivu na si vyenginevyo huku akishangazwa na chama cha CUF kutotaka amani na kuwaeleza vijana vijana kuwa hakuna chama chengine cha kukiunga mkono isipokuwa CCM

Nae Waziri wa Maji,Ardhi na Nishati Ramadhani Abdalla Shaaban aligusia suala la mafuta na gesi ambalo limekuwa likipotoshwa na viongozi wa CUF na kusema kuwa chama hicho kinafanya hivyo kwa sababu hakina hoja za msingi za kuwaambia wananchi wa Pemba kutokana na maendeleo makubwa yaliopatikana.

No comments:

Post a Comment