Monday, 28 December 2015

CCM YAJIANDAA KUSHINDA UCHAGUZI MKUU WA MARUDIO ZANZIBAR KWA KISHINDO



NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimewataka wana CCM kujiimarisha, kujiweka tayari na kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio, ili kukiletea ushindi wa kishindo chama.

Aidha kimeridhia majadiliano yanayoendelea kuhusu hali ya kisiasa Zanzibar, yanayoshirikisha viongozi kadhaa, wakiwemo marais wastaafu Ali Hassan Mwinyi, Dk. Salmin Amour Juma na Amani Abeid Karume, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi.

Katibu wa Kamati Maalum wa NEC, Idara ya Itikadi na Uenezi ya CCM, Zanzibar, alitoa msimamo huo jana, baada ya kumalizika kwa kikao cha Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Zanzibar.

Alisema chama kinawataka wanachama wake, kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi wa marudio kuanzia rais, wajumbe wa Baraza la Wawakilishi na madiwani wakati utakapofi ka. Waride alisema kikao hicho kiliongozwa na Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Rais Dk. Ali Mohamed Shein na kwamba kilikuwa cha kawaida cha siku moja, ambacho kilifanyika Ofi si Kuu ya Chama, Kisiwandui Mjini Unguja.

Alisema kikao hicho pamoja na mambo mengine, kimempongeza kwa dhati Dk. Joh Magufuli kwa kuchaguliwa katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 25, 2015 kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, baada ya kupata ushindi wa kishindo. Waride alisema kikao hicho kimempongeza Samia Suluhu Hassan kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Alisema kikao kimefurahishwa, kuridhishwa na kufarajika na idadi kubwa ya wana CCM kwa kujitokeza kwa wingi katika uchaguzi mkuu. Waride alisema kikao kimepongeza juhudi zinazochukuliwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar   (SMZ), chini ya uongozi wa Rais Dk. Shein katika kuwaletea maendeleo ya kiuchumi na kijamii wananchi.

Alisema kikao hicho kinampongeza Dk. Shein kwa kusimamia suala la amani na utulivu wa nchi kwa kipindi chote cha miaka mitano iliyopita.

Waride alisema mbali na hilo, serikali imetakiwa kuongeza juhudi na kubuni mikakati madhubuti itakayosaidia kwa kiasi kikubwa kuanzishwa kwa miradi mipya ya maendeleo mijini na vijijini ili kuinua mapato ya taifa.

Hata hivyo alisema kikao hicho kimetoa pongezi za pekee kwa wajumbe wote wa Kamati Maalum ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, viongozi wa Chama na Jumuiya zake kwa kazi nzuri ya kuimarisha Chama na kuwataka kuwa mstari wa mbele katika kukipigania, kukilinda na kukitetea  kwa nguvu zote.

Aidha, kimewataka kuendelea kufanya kazi kwa mashirikiano, juhudi na maarifa katika  kukijenga na kukiimarisha Chama kwa maslahi ya Wazanzibari na Watanzania kwa ujumla. Matokeo ya uchaguzi wa Zanzibar, yalifutwa Oktoba 28, mwaka huu, na Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jecha Salum Jecha baada ya kubaini kasoro kadhaa

No comments:

Post a Comment