Saturday, 26 December 2015
MAJALIWA AWATAKA WATANZANIA KUENDELEZA AMANI ILIYOPO
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akiwasili katika Viwanja vya Karim Jee jijini Dar es Salaam katika sherehe za Maulid. (Picha na Raymond Mushumbusi Maelezo)
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akifurahi jambo, alipokuwa akishiriki katika sherehe za Maulid (Kushoto) Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Bin Zuberi Bin Ali na kulia ni Rais Msataafu wa Awamu ya Pili Ali Hassan Mwinyi
Na Raymond Mushumbusi MAELEZO
Watanzania wameaswa kuiendeleza amani na utulivu iliyopo kwa sasa nchini na kutoiacha ikapotea kwani ndio nguzo muhimu kwa watanzania na mstakabali wa maendeleo ya nchi yetu kiujumla.
Hayo yamesemwa leo na Waziri Mkuu Mhe Kassimu Majaliwa alipokuwa akihutubi Baraza la Maulid lililofanyika katika viwanja vya karim Jee Jijini Dar es salaam na kuwaasa waislamu wote nchini na watanzania kiujumla kudumisha upendo amani na mshikamano uliopo.
Waziri mkuu Kassimu Majalimu ameongeza kuwa serikali itaendelea kushirikiana na Taasisi za kidini katika kulenda maendeleo na kutoa huduma kwa wananchi ikiwemo Elimu na Afya.
Pia ameitaka jamii ya kislamu na watanzania wote kuzingatia maadili mema na kuwafundisha watoto maadili mazuri ili kupunguza wimbi la uvunjivu wa maadili nchini ambao unasababisha vijana wengi kupotea katika madawa ya kulevya na kupata mimba za utotoni.
“Sisi kama Serikali ya Awamu ya Tano tuko makini sana na tunatoa shukrani kwa Baraza la Kuu la Waislamu Tanzania (BAKWATA) kwa kushirikiana na sisi katika maswala mbalimbali ya kimaendeleo na sisi tutashirikiana nanyi bega kwa bega”alisema Waziri Mkuu Majaliwa.
Naye Sheikh Mkuu wa Tanzania Mufti Abubakari Bin Zuberi Bin Ali amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Awamu ya Tano na kumpongeza pia kwa kumteuwa Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa na kuteuwa mawaziri makini katika kuiletea maendeleo nchi yetu.
Waislamu wote Duniani leo wanaikumbuka siku ya kuzaliwa Mtume wao Mohamed SAW na kwa Tanzania maadhimisho hayo yamefanyika kitaifa katika viwanja vya Karim Jee Jijini dare s salaam nakuhudhuriwa na viongozi wa chini dini, na mabalozi mabalimbali waislamu na wanachi wa dini zote.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment