Saturday, 26 December 2015

NIOMBEENI- MAGUFULI



 Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli, mkewe Mama Janeth Magufuli na Mke wa Rais Mama  Janeth Magufuli  wakishiriki Ibada ya Krismas katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015




Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akisalimiana na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam aliyemkaribisha kusalimia wananchi bada ya kumalizika kwa Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015
Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akitoa salamu zake za heri ya Krismasi mara baada ya kumalizika Ibada ya Krismas misa ya kwanza katika Kanisa la Mtakatifu Peter jijini Dar es salaam leo Desemba 25, 2015

Rais Dkt John Pombe Joseph Magufuli akizungumza na Muadhama Askofu Mkuu Polycarp Kardinali Pengo wa Jimbo Kuu la Dar es Salaam kushoto ni Mke wa Rais Mama Janeth Magufuli.
Mwadhama Askofu mkuu Kadilanali Polycarp  Pengo akitoa mahubiri yake wakati wa ibada hiyo ya Krismas kwenye Kanisa la Saint Peter Oysterbay jijini Dar es salaam.

NA MWANDISHI WETU

RAIS Dk. John Magufuli ameungana na Wakristo wengine duniani kushiriki katika Misa ya Krismas, huku akiwataka kuishi kwa amani na utulivu kwa kufuata mienendo aliyokuwa nayo Yesu Kristo.

Pia, amewataka waumini wa Kikristo na wasiokuwa Wakristo wafanye kazi kwa bidii ili watekeleze falsafa ya Hapa Kazi Tu kwa vitendo kwa kuwa hata manabii akiwemo Yesu Kristo alikuwa anapenda kufanya kazi shukrani kanisani hapo.

Wakati wote akiwa katika kanisa hilo, Rais Dk.Magufuli, alionekana mwenye furaha huku akisalimiana na waumini wenzake na kuwataka wadumishe sikukuu hiyo kwa kuishi kwa amani na upendo miongoni mwao.

“Ni Sikukuu muhimu kwetu na tunapaswa tusherehekee kwa amani na upendo miongoni mwetu kwa kuwa ni moja ya jambo muhimu kwetu kama Watanzania,”alisema.

Aidha, aliwaomba waumini hao kumuombea yeye na Watanzania wote ili aendelee kutimiza ahadi alizowaahidi katika kuwatumikia kwa kuwa kazi aliyopewa ni kubwa.

Katika hatua nyingine, watoto 32 wamezaliwa wakati wa mkesha wa Sikukuu ya Krismas, katika Hospitali ya Rufani Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Kitengo cha Wazazi Meta na Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mbeya, iliyopo Forest mpya, mjini hapa.

Kati ya watoto hao, 14 wamezaliwa kwa njia ya upasuaji na hali zao pamoja na mama zao zinaendelea vizuri. Muuguzi wa zamu katika kitengo cha Wazazi Meta, Fatuma Mkinga, alisema jumla ya watoto 24 wamezaliwa katika kitengo hicho, kilicho chini ya hospitali ya Rufani Kanda ya Nyada za Juu Kusini iliyopo mjini Mbeya (zamani ikijulikana kwa jina hospitali ya Rufani Mbeya).

Fatuma alisema watoto 13 wamezaliwa kwa njia ya kawaida, wakati wale waliozaliwa kwa upasuaji ni 11. “Watoto wote wakiwemo hawa 11 waliozaliwa kwa upasuaji, wanaendelea vizuri. Watoto wa kiume wapo 14 wakati wa kike ni 10,”alisema Fatuma.

Naye Muuguzi katika Hospitali ya Rufani ya Mkoa wa Mbeya, Atu Kiswaga, alisema jumla ya watoto waliozaliwa katika mkesha wa Krismas ni wanane.

Atu alisema watoto watatu wamezaliwa kwa njia ya upasuaji wakati waliosalia wamezaliwa kwa njia ya kawaida, na kwamba wa kike wapo saba huku mtoto wa kiume akiwa ni mmoja. Alisema hali za watoto hao na mama zao ni nzuri

No comments:

Post a Comment