Saturday 30 April 2016

NDUGAI AKABIDHI USPIKA WA MABUNGE YA AFRIKA MASHARIKI



Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai akimkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake. Alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016. Kulia ni Katibu wa Bunge Dkt Thomas Kashililah

Na Mwandishi wetu

Spika wa Bunge Mhe. Job Ndugai amemkabidhi Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe. Daniel Kidega baada ya Tanzania kumaliza muda wake.

Spika Ndugai alimkabidhi Uenyekiti huo wakati wa Mkutano wa kumi na moja (11) wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za Afrika Mashariki uliofanyika Jijini Arusha leo tarehe 29 Aprili, 2016.

Mkutano huo pia ulihudhuriwa na Spika wa Bunge la  Seneti la Kenya, Spika wa Bunge la Kenya, Rais wa Bunge la Seniti la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Burundi, Naibu Spika wa Bunge la Rwanda, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki pamoja na Makatibu wa Mabunge ya nchi wanachama wa Afrika Mashariki.

Akiukabidhi Uenyekiti huo Spika Ndugai aliwashukuru Maspika wenzake kwa ushirikiano walimuonesha katika kipindi chote cha  Uongozi wake na kumtakia kila la kheri Mwenyekiti  mpya wa jukwaa hilo.

Maspika wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki hushika Uenyekiti wa Jukwaa la Maspika wa Jumuiya hiyo kwa kipindi cha mwaka mmoja ambapo Tanzania ilichukua Uenyekiti wa Jumuiya hiyo mwaka jana.

Spika wa Bunge la Afrika Mashariki Mhe Kidega atashiki Uenyekiti wa Jukwaa hilo kwa kipindi cha mwaka mmoja kabla ya kuukabidhi kwa Spika mwingine katika mkutano ujao unaotarajiwa kufanyika nchini Kenya.

Pamoja na mambo mengine mkutano huo wa Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki ulijadili maswala mbalimbali yanayohusiana na nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Jukwaa la Maspika wa Mabunge ya nchi za  Jumuiya ya Afrika Mashariki lilianzishwa mwaka 2008.

No comments:

Post a Comment