Tuesday 19 April 2016

DARAJA LA KIGAMBONI SASA KUITWA DARAJA LA NYERERE

RAIS Dk. John Magufuli ameamua kulibadili jina Daraja la Kigamboni, ambapo sasa litajulikana kwa jina la Daraja la Nyerere.

Rais Magufuli alitangaza uamuzi huo leo wakati akiwahutubia mamia ya wananchi wakati wa uzinduzi wa daraja hilo, uliofanyika maeneo ya Kurasini, Dar es Salaam.

Alisema amepata wazo hilo kutokana na mchango mkubwa uliotolewa na Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere, katika kupigania Uhuru wa Tanganyika, kuziunganisha Tanzania Bara na Zanzibar na hatimaye kuwaunganisha Watanzania bila kujali rangi, dini na makabila.

Rais Magufuli alisema hakuona sababu ya daraja hilo kupewa jina lake kama baadhi ya watu walivyopendekeza, wakati wapo watu waliofanyakazi kubwa ya kuijenga Tanzania, ambayo hadi sasa inasifika kwa kuwa nchi ya amani na utulivu.

No comments:

Post a Comment