Tuesday 30 August 2016

CUF SASA YAMEGUKA VIPANDE, IPO CUF YA BARA NA YA VISIWANI



HALI ndani ya chama cha CUF si shwari, kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ubabe unaofanywa na Katibu Mkuu wake, Seif Sharif Hamad wa kumfukuza uanachama kila asiyeunga mkono uamuzi wake, kama chama hicho ni mali yake.
Hatua hiyo inafuatia Baraza Kuu la chama hicho kutangaza kuwasimamisha wanachama 11, akiwemo aliyekuwa Mwenyekiti wake taifa, Profesa Ibrahimu Lipumba na kumfukuza Mwenyekiti wa Baraza la Wazee.
Baadhi ya wajumbe waliotimuliwa wamesema Maalim Seif anataka kugeuza CUF kijiwe cha majungu, fi tna, unafi ki na nongwa kwani anafanya kazi kwa maslahi ya tumbo lake, ikiwemo
kutumiwa na CHADEMA kuua CUF ili kibaki chama kimoja bara.
Walisema Profesa Lipumba alijiuzulu kwa ajili ya kukilinda chama katika wakati mgumu wa uchaguzi kwa kuwa Maalim Seif alikisaliti na kukubali fungu
kutoka CHADEMA.
Wanachama hao wamempongeza Rais wa Zanzibar Dk. Ali Mohamed Shein kwa uvumilivu wa kufanya kazi na Maalim Seif kwa kuwa ni vigumu kuishi na kufanya nae kazi.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi wa wanachama hao kwa sharti la kutotajwa majina, walisema CUF ilipofi kia inahitaji watu kujitoa ili kukinusuru na lazima wajitoe kwa kuwa uvumilivu kwa Maalim Seuf umefi kia mwisho.
Baadhi ya waliodaiwa kusimamishwa au kufukuzwa ndani ya chama hicho walisema hadi sasa hakuna aliyepata barua rasmi ya kufukuzwa, ila ni porojo na nongwa za kufanya kazi nje ya uamuzi wa kikatiba.
“Sisi tunaona kinachofanyika ni uhuni na aibu kwa watu ambao wanafanya siasa za uchochezi kwa kudai wanapinga udikteta, huku wao wakiwa ni madikteta waliopitiliza…. mtu anaamka ili kulinda tumbo lake akiwa na maslahi kuona CUF inakufa bara na kubaki CHADEMA yenye nguvu, anafukuza watu na kusimamisha kiholela,”alisema mmoja wao.
Alisema hatua ya kujiuzulu kwa Profesa Lipumba ilifunikwa ili kulinda maslahi ya chama kuelekea katika uchaguzi mkuu na wanachama watambue hakuna chama kimefanya uchaguzi katika wakati mgumu kama CUF, kwa kuwa Maalim Seif alikuwa msaliti na alichukua fungu kubwa la pesa ili kufanya kampeni Zanzibar na kutaka bara iachiwe CHADEMA.
Chanzo kingine cha habari kilisema
katibu mkuu huyo wa CUF anaongoza chama kama mungu mtu, hataki kuhojiwa wala kuulizwa hata kama anachokifanya hakina maslahi kwa chama.
“Profesa Lipumba ana mengi, Maalim ni mtu ambaye hataki kuguswa, wala kuulizwa, sasa tunamhakikishia atufukuze, atuache tutaendelea kumwuunga mkono Profesa Lipumba kwa maslahi ya chama si ya tumbo lake na CHADEMA,”kilisema chanzo hicho.
Alisema uongozi wa kidikteta unaofanywa na Maalim Seif umesababisha kufanya vikao viwili Zanzibar baada ya kuvunjika mkutano mkuu bila kushirikisha baadhi ya wajumbe wa kamati kuu na halmashauri kuu.
Alisema wanasikitika katika kipindi cha uongozi wa Maalim Seif akiwa Makamu wa Rais Zanzibar, chama cha CUF hakikunufaika na chochote na hata
alipokuwa akifika Dar es Salaam, alifikia katika hoteli ya Serena na kuwasiliana na vibaraka wake na kuwaita kimyakimya ili wampe taarifa za majungu.
Naibu Katibu Mkuu wa CUF (Bara) Magdalema Sakaya, ambaye ni Mbunge wa Kaliua, alipoulizwa kuhusiana na mgogoro huo, alisema hana majibu ya kina kwa kuwa hata naye anatajwa kusimamishwa, japo hana taarifa za kiofisi.
Alisema juzi usiku alitumiwa ujumbe mfupi wa simu (sms) kwa namba ya simu ya mkononi na mwandishi wa mikutano wa CUF, anayejulikana kwa jina la Shamte, kuwa ameagizwa amjulishe kutakuwa na kikao cha Baraza Kuu Zanzibar ambacho kitatanguliwa na kikao cha utendaji.
“Nilivyoona ile sms usiku nilishangaa…mimi ndiyo Naibu Katibu Mkuu Bara, ambaye ndiye mtendaji mkuu, ukimuondoa Katibu Mkuu, lakini sms ya kikao ninatumiwa na mtu mdogo, mhudumu ndani ya chama, tena kuhusu kikao kizito cha uamuzi ni
taasisi gani inaendeshwa hivyo? alihoji Magdalena.
Alisema awali alipuuza sms hiyo na kudhani imepotea njia, lakini aliona haja ya kuwasiliana na Maalim Seif ambapo alimpigia bila mafanikio.
Magdalena alisema baada ya mawasiliano hayo kukwama, alimtumia sms kuwa: “Nimetumiwa sms ya kikao na mwandishi wa chama, lakini si utaratibu wa taasisi ukizingatia mimi ndiyo msaidizi wako mkuu.”
Anasema baada ya ujumbe huo alijibiwa: “ Ni kweli kutokan ana umuhimu wa kikao njoo ni dharura.
Alisema aliendelea kumtumia sms na kuhoji kuhusu wajumbe wa mkoani ambao wana haki ya kikatiba kuudhuria mkutano huo wa dharura wa chama wa uamuzi, akanijibu kuwa nasisitiza wafike.
Baada ya majibu hayo, Magdalena alisema aliona hiyo ni dharau na kuna agenda za siri katika mkutano huo, hivyo hakuhudhuria na kuwa baadaye jana, alifahamishwa wanachama 11 wamesimamishwa na mmoja kafukuzwa.


Kwa upande wake, Maftaha Nachuma (Mtwara Mjini – CUF) alisema amesikia taarifa za kusimamishwa au kufukuzwa, lakini anawahakikishia wananchi kuwa hakuna kitu kama hicho kwa kuwa CUF inaendeshwa kwa kufuata katiba, hivyo hawezi kufukuzwa bila kuhojiwa au kupewa barua.
“CUF ni taasisi, ikitokea nikapewa barua najiamini sina kosa na hakuna uwezo wa kufukuza nje ya katiba bila kusikilizwa, kuhoji, demokrasia ni haki ya kila mwanachama, si dhambi kama kosa ni kumtaka Lipumba na kumpenda, hatutarudi nyuma…nasubiri nikipewa barua nitaongea na tuna mengi,”alisema Nachuma.
Wingu la kusambaratika kwa CUF linaendelea kukiandama chama hicho, ambapo kila uchwao kunaibuka fi gisufi gisu ndani yake ambazo zikiangaliwa vizuri, zilichochewa kwa kiasi kikubwa na vyama vingine vya upinzani ambavyo vinanufaika CUF
ikikosa utulivu.
Baada ya uchaguzi mkuu, wakati ambao kiuhalisia Ukawa iliyeyuka, taarifa zinasema CUF ilijitahidi kujiimarisha, lakini bado Maalim Seif alitumika kuhakikisha kuwa hakisimami na Profesa Lipumba harudi kwenye nyadhifa yoyote kwa madai kuwa ni msaliti.
Mbali ya kumvua uanachama Profesa Lipumba na kumsimamisha Magdalena Sakaya na mbunge Nachuma, wengine waliovuliwa uanachama ni Mjumbe wa Baraza Kuu na Katibu wa CUF Wilaya ya Handeni, Masoud Mhina, Mjumbe wa Baraza Kuu, Ashura Mustapha.
Wengine ni Naibu Mkurugenzi wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, Abdul Kambaya, Haroub Shamis, Mohamed Habib Mnyaa, Thomas Malima, Kapasha Kapasha na Musa Haji Foum.
Akieleza kuhusiana na uamuzi huo wa CUF, Kambaya kupitia ukurasa wake wa facebook, aliandika jana asubuhi kuwa amekuwa akipigiwa simu nyingi kutoka kwa watu mbalimbali kuhusu hatua iliyofi kiwa dhidi yake.
Alisema yeye na wenzake ikiwa ni Pamoja na Wabunge wa Mtwara Mjini (Maftaha Nachuma) na Magdalena
Sakaya wa Jimbo la Kaliua, Diwani wa Kata ya Misima Wilayani Handeni na wale ambao wametajwa hawakuwepo wakati hukumu hiyo inatolewa na Baraza Kuu lililofanyika Zanzibar.
Hata hivyo, alisema baada ya kuahirishwa kwa mkutano mkuu uliofanyika Ubungo Plaza, Agosti 21, mwaka huu, kutokana na wajumbe 324 kutoridhishwa na ukiukwaji wa Katiba ya chama chao, ikiwa ni pamoja na kuingizwa kwa wajumbe wasio halali, yeye alikuwa miongoni mwa wajumbe waliojiojiorodhesha na kuandika barua ya malalamiko, kisha kuipeleka Ofi si ya Msajili wa Vyama.
Alisema kutokana na hayo, uamuzi wa Baraza la CUF dhidi yao hata kabla ya kutoa majibu ya hoja zao walizowasilisha kwa msajili ni wazi kuwa hawana majibu sahihi ya hoja zao.
“Na jambo hili sio geni kwa hapa duniani, Firauni aliposhindwa kuthibitisha kuwa yeye ndiye Mungu, alitumia Jeshi lake (Baraza Kuu) kutaka kumuangamiza Mussa na wafuasi wake waliokuwa wanaamini katika haki na Mungu wa kweli, kwa hiyo kilichoendelea Zanzibar ni mfano hai wa Firauni na jeshi lake dhidi ya Mussa na wafuasi wake,” alisema.
Aliongeza kuwa: “Kauli yangu ya mwisho ni kwamba hatoki mtu kwenye CUF hii kwa kuwa si mali ya mtu bali ni ya watu, si jambo jema kujifananisha na Firauni, jibu hoja usitumie jeshi kujibu hoja. Hakuna kukata tamaa, wala kukimbia CUF. Harakati za kutafuta uhuru ndani ya chama changu kwa Watanganyika ndiyo kwanza umezifungulia geti, sasa ni hoja za makabwela dhidi ya vibaraka wa mabepari wa Tanganyika.”
Profesa Ibrahim Lipumba ambaye aliwahi kuwa Mwenyekiti wa chama hicho, alijiuzulu nafasi hiyo katikati mwa mwaka jana wakati wa vuguvugu la uchaguzi mkuu kwa madai kuwa dhamira inamsuta kumpokea Edward Lowassa kuwa miongoni mwa umoja wao wa Ukawa.
Akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam, Agosti mwaka jana, Profesa Lipumba alisema amejitahidi kujenga
chama hicho hasa Tanzania bara, amejenga umoja wa Wazanzibari, hivyo anajiuzulu kulinda heshima yake.
Alisema ameikabidhi Ofisi ya Katibu Mkuu, barua yake ya kung'atuka nafasi ya Mwenyekiti wa Taifa, lakini ataendelea kuwa mwanachama wa CUF na kadi yake imelipiwa mpaka mwaka 2020.
Alieleza sababu za kujiuzulu ni umoja wa huo wa Ukawa kushindwa kuenzi Tunu za Taifa katika umoja wao kwa kuwakaribisha watu waliopitisha rasimu iliyochakachuliwa kwenye Bunge Maalumu la Katiba.
WAZEE WA CUF WAFUNGUKA
Umoja wa Wazee wa CUF wa Mkoa wa Dar es Salaam, walizungumza na waandishi wa habari jana na kudai walichukua hatua kadhaa kushauri juu ya kadhia iliyopo ndani ya CUF bila mafanikio.
Kupitia kwa Katibu wao, Abdul Magomba, walisema viongozi wa CUF wamekosa ushirikiano mwema, wamejaa kiburi, jeuri na ubinafsi, jambo lililozaa mambo yaliyotokea Ubungo Plaza, juma lililopita.
Alisema kutengwa kwa baadhi ya viongozi na kuporwa kwa majukumu yao ya kiutendaji ndani ya chama, kutokubali ushauri wa wazee Kuhusu kumaliza kile kinachoitwa mgogoro wa kujiuzulu Profesa Ibrahim Haruna Lipumba, ndiyo chanzo kikubwa cha mpasuko ndani ya CUF.
“Sisi wazee wa mkoa wa Dar es Salaam, tumeona kuna mkakati wa makusudi unaofanywa na Katibu Mkuu wetu, Maalim Seif Shariff Hamad wa kukiua chama cha CUF kwa upande wa Tanzania Bara. Hakuna tatizo la kikatiba katika kumaliza mgogoro huo kwa sababu ibara ya 117 kifungu cha 1 na 2 kinaeleza vyema utaratibu wa Kujiuzulu, na kwa kweli wajumbe wa mkutano mkuu walitekeleza Wajibu wao,” alisema
Mzee Abdul.
Hata hivyo aliongeza kuwa: “Sisi wazee tunapenda kuwajulisha Watanzania kwamba, tulikutana na katibu mkuu na tumemsihi sana amalize tatizo la
Profesa Lipumba, lakini kama tulivyosema hapo awali, kwamba kiburi, dharau na jeuri ndiyo vimetufi kisha hapa.”
Alisema wajumbe 324 waliwasilisha madai yao kwa Msajili wa Vyama vya Siasa kupinga ubeberu unaondelezwa ndani ya CUF na katibu mkuu na kwamba wao kama wazee wa chama mkoa wa Dar es Salaam wanaunga mkono uamuzi hayo ya wajumbe.
Alimtaka msajili kushughulikia tatizo hilo kwa mujibu wa katiba yao kwa sababu ni fedheha kubwa kwao wanaodai kuhubiri demokrasia, kuiminya demokrasia hiyo ndani ya chama chao wenyewe.
Kuhusu kikao kilichoitishwa jana na Maalim Seif kwa kushirikiana na viongozi wa Zanzibar pekee, bila kushirikiana na viongozi wa Bara, wazee wa mkoa wa Dar es Salaam walisema kutokana na uzoefu wa kilichotokea kwenye mkutano mkuu uliofanyika Ubungo Plaza, waliamua kuwakataza wajumbe wa Baraza Kuu upande wa Bara, ambao wamejitoa mhanga kupinga Ubeberu, kutohudhuria vikao hivyo kutokana na kukosa uhakika wa usalama wa wajumbe hao

No comments:

Post a Comment