Mkuu wa wilaya ya Bukoba Mh. Deodatus Kinawiro amethibitisha kufariki kwa watu 11 na wengine 196 kujeruhiwa katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera kufuatia lenye tetememko la ardhi ukubwa wa vipimo vya 5.7 lililotokea moani humo na kusababisha madhara makubwa.
Akizungumza na mtandao huu kwa njia ya simu amesema tetemeko lililotokea mchana leo lilikuwa ni kubwa na limeathiri majengo mengi na kusababisha majeruhi na vifo, hata hivyo bado Kamati ya Ulinzi na Usalama ikishirikiana na vikosi vya uokoaji pamoja na majeshi la ulinzi na usalama vinaendelea kufanya tathmini ya uharibifu wa majengo na mali uliosababishwa na Tetemeko hilo.
DC Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitaendeleo kutolewa kadri zitakavyopatikana kutokana na kuendelea kwa kazi ya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.
DC Kinawiro ameongeza kwamba taarifa zaidi zitaendeleo kutolewa kadri zitakavyopatikana kutokana na kuendelea kwa kazi ya tathmini ya athari ya tetemeko hilo.
No comments:
Post a Comment