Tuesday 20 December 2016

SERIKALI YAFANYA UTEUZI WA MAKATIBU TAWALA WA WILAYA

SERIKALI imefanya uteuzi wa makatibu tawala wa wilaya 27 nchini ili kujaza nafasi zilizokuwa wazi.

Walioteuliwa kujaza nafasi hizo, kituo cha kazi kikiwa kwenye mabano ni Timotheo Mzava (Arumeru), Fabian Sospeter (Nyanghwale),
Innocent Nsena (Karagwe), Abdalla Mayomba (Missenyi), Greyson Mwengu (Kyerwa) na Agness Alex (Biharamulo).

Wengine ni Sarah Sanga (Hanang), Paul Bura (Mbulu), Mbwana Kambagwa (Liwale), Agnellus Mwakitalu (Kilwa), Yohana Kasitila (Kilosa), Robert Selasela (Kilombero) na Lameck Lusesa (Malinyi).

Wateuliwa wengine ni Palango Abdul (Nanyumbu), James Bugali (Misungwi), Menruf Nyoni (Magu), Saidi Kitinga (Ilemela),
Grace Mgeni (Makete), Zaina Mlawa (Ludewa), Milongo Sanga (Kibiti).

Makatibu tawala wengine wapya ni Frank Sichalwe (Kalambo), Nicodemus Mwikozi (Meatu), Filbert Kanyilizu (Itilima), Godwin Chache (Busega), Winfrida Emmanuel (Ikungi), Elizabeth Rwegasira (Mkalama) na Michael Nyahenga (Kaliua).

Taarifa iliyotolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma    na Utawala Bora, ilisema makatibu tawala hao wanatakiwa wafike ofisini kwa katibu mkuu wakiwa na CV zao pamoja na nakala za vyeti vyao vya kielimu.

No comments:

Post a Comment