Wednesday, 15 March 2017
MAKONDA AAGIZA NYUMBA 36 ZIBOMOLEWA DAR
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, ameagiza kuvunywa kwa nyumba 36, ambazo zimejengwa kwenye maeneo hatarishi, hasa mabondeni bila fidia katika Kata ya Vingunguti, Manispaa ya Ilala.
Nyumba hizo zinatarajiwa kuvunjwa leo, baada ya baadhi ya wamiliki wa kudaiwa kuuza viwanja walivyopewa eneo la Mabwepande, huku wengine wakipangisha nyumba hizo, ambazo awali walitakiwa kuzivunja.
Katika ziara aliyofanya jana, kwenye maeneo yaliyokumbwa na mafuriko, Makonda aliiagiza manispaa chini ya mkuu wa wilaya, ambaye ni mwenyekiti wa kamati ya maafa, kubainisha nyumba hizo na kuzibomoa bila kutolewa kwa fidia.
Pia, Makonda aliwaagiza wananchi hao kuwa walinzi wa miundombinu kutokana na baadhi ya wakazi wa maeneo hayo kuchimba vyoo na mchanga katika eneo la mkondo wa maji na kuhatarisha maisha ya wakazi hao pindi mvua zinaponyesha.
"Tabia zetu na uchafu ndio zinasababisha mto huu kujaa takataka na hata miundombinu serikali inayotengeneza itazidi kuharibika, lakini bado watu wanajenga nyumba katika mfereji na wanataka serikali iwalipe,”alionya Makonda.
Aidha, alitangaza ujenzi wa Daraja la Mto Msimbazi kupitia msaada wa fedha utakaotolewa na Benki ya Dunia (WB), baada ya wakazi wa mtaa huo wa Mji Mpya na Vingunguti, kulalamikia adha wanayopata kutokana na ukosefu wa daraja.
Baadhi ya wakazi hao walikiri kuishi maeneo hayo ya bondeni kutokana na gharama za nyumba za kupanga kuwa chini tofauti na maeneo mengine.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment