Sunday 30 April 2017

RAIS MAGUFULI AWATAKA WAFANYAKAZI 9932 WALIOGHUSHI VYETI KUONDOA MAENEO YA KAZI MARA MOJA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amewataka watumishi 9932 waliogushi vyeti, kuondoka maeneo yao ya kazi haraka iwezekanavyo kabla hawajadhibiwa kwa mujibu wa sheria.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo mjini Dodoma alipokuwa akikabidhiwa taarifa ya uhakiki wa vyeti vya watumishi wa umma sambamba na uzinduzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Chuo Kikuu cha Dodoma (UDOM).
“Watumishi 9932 wenye vyeti vya kugushi na feki mishahara yao ya mwezi huu ikatwe na waondoke kazini mara moja na hizo nafasi zitangwazwe ili wasomi waweze kuziomba na majina yao yawekwe kwenye magazeti ili wajulikane” amesema Rais Magufuli
Aidha amesema kuwa hadi kufika tarehe 15 Mei, 2017 kila mkuu wa Idara mahali pake pa kazi ahakikishe watumishi hao wameondoka na watakao kaidi agizo hilo amevitaka vyombo vya usalama kuwashughulikia.
Hata hivyo Rais Magufuli ameongeza kuwa watumisi 1538 wanaotumia cheti zaidi ya mtu mmoja kutopewa mshahara hadi pale itakapojulikana nani mwenye cheti halali na kuwataka watumishi 11,769 kuwasilisha vyeti vilivyopungua.
Mbali na hayo Rais Magufuli amewataka wanafunzi kusoma kwa bidii na kuachana na masuala ya siasa kwa lengo la kujenga nchi kwani watanzania wanahitaji maendeleo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma Angela Kairuki amesema kuwa mpaka sasa vyeti vilivyohakikiwa ni 435,000 ambapo imefanyika kwa awamu tatu iliyojumuisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali pamoja na Serikali Kuu.
“Leo tunakabidhi taarifa ya awamu mbili iliyohusisha Serikali za Mitaa, Taasisi na Mashirika ya Umma, Tume na Ofisi ya Menejimenti ya Utumishi na Wakala wa Serikali ambapo imejumuisha uhakiki wa vyeti vya Kidato cha Nne, Sita, vyeti vya ualimu kwa ngazi ya cheti na stashahada” amesema Waziri Kairuki.
 Amesema kuwa matokeo ya uhakiki wa vyeti kwa watumishi wa umma yapo ya aina nne ambapo watumishi 376,969 sawa na asilimia 94.23 wanavyeti halali, watumishi 9932 asilimia 2.4 wanavyeti vya kugushi, watumishi 1538 asilimia 0.3 vyeti vyao  vinatumika kwa zaidi ya mtu mmoja na watumishi 11,769 asilimia 2.8 wanavyeti pungufu.
Nae Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako alisema wizara yake inakumbana na changamoto ya watumishi wa umma kugushi vyeti hivyo aliwataka wanafunzi kusoma kwa bidii kwani serikali imeziba njia zote za mkato za kuajiriwa na Serikali.
“Leo tunaandika historia ya kipekee kwani suala la uhakiki wa yveti limefanyika kwa mara ya kwanza nchini ambapo Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ndio yenye jukumu la kuhakiki uhalali wa vyeti hivyo” amesema Prof. Ndalichako.
Zoezi la uhakiki wa vyeti kwa Watumishi wa Umma limeendeshwa na Serikali ya Awamu ya Tano kuanzia Mwezi Oktoba, 2016 likiwa na lengo la kubaini uhalali wa vyeti kwa watumishi wake.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli  akiionyesha Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma kwa wananchi waliohudh,.uria uzinduzi wa Taarifa hiyo katika ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma,Kushoto kwake  ni Makamu wa Rais Mhe.Samia Hassan Suluhu na Kulia kwake ni Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)Prof.Idris Kikula.

 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli   na Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu wakifwatilia Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma mara baada ya kuizindua katika Viwanja vya Chimwaga Mjini Dodoma leo.Kushoto kwa Makamu wa Rais ni Waziri nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI Mhe.George Simbachawene.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli ,Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu na Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa wakibonyeza kitufe kuzindua wiki ya Maandimisho ya Miaka 10 ya Chuo  kikuu cha Dodoma(UDOM).

Wananchi mbalimbali wakifuatilia Hotuba ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.John Pombe Magufuli wakati akipokea Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma katika viwanja vya Chimwaga Mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli   akihutubia wananchi katika Ukumbi wa Chimwaga Mjini Dodoma leo kabla ya kupokea Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma.

Waziri Mkuu Mhe.Kassima Majaliwa akitoa salamu kwa wananchi waliofika katika ukumbi wa Chimwaga leo Mjini Dodoma.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli  akipokea Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma kutoka kwa Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angela Kairuki katika Ukumbi wa Chimwaga,Mjini Dodoma.

Viongozi mbalimbali waliohudhuria Hafla hiyo wakiwa katika ukumbi wa Chimwaga wakisubiri upokeaji wa Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma leo Mjini Dodoma.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli  akizungumza jambo na Makamu wa Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)Prof.Idris Kikula kabla hajapokea Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma.

Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu akizungumza katika hafla ya upokeaji wa Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma Mjini Dodoma leo.


Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Job Ndugai,Waziri Mkuu Mhe.Kassim Majaliwa na Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Mhe.Prof,Joyce Ndalichako wakifuatilia hotuba ya Rais wa jahuri ya Muungano wa Tanzania wakati wa upokeaji wa Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma Mjini Dodoma leo.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe,John Pombe Magufuli, akikata utepe kuzingua Taarifa ya Uhakiki wa Vyeti kwa watumishi wa Umma Mjini Dodoma leo.Wengine pichani Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu, Waziri wa Nchi,Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angela Kairuki na Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dodoma(UDOM)Prof.Idris Kikula.

Picha zote na Daudi Manongi-MAELEZO,DODOMA


No comments:

Post a Comment