Thursday, 24 August 2017

HATMA YA MANJI KESHO


KESI ya kukutwa na dawa za kulevya, inayombili mfanyabiashara Yussuf Manji, imepangwa kutolewa uamuzi kesho iwapo ana kesi ya kujibu au la.

Hatua hiyo imekuja baada ya upande wa jamhuri kufunga ushahidi, baada ya kumalizika kwa usikilizwaji wa mashahidi watatu.

Manji alipanda kizimbani jana, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha, wakati shauri hilo lilipopelekwa kwa ajili ya kuendelea na ushahidi wa upande wa mashitaka.

Akitoa ushahidi wake, mkemia kutoka ofisi ya Mkemia Mkuu wa Serikali, Domician Dominic, akiongozwa na Wakili wa Serikali Mkuu, Timon Vitalis, alidai kuwa matokeo ya uchunguzi wa mkojo yalikutwana na kemikali aina ya
benzodiazepines na morphine.

Shahidi huyo alidai kuwa, kemikali hizo hutumika hospitali kwa ajili ya mgonjwa, ambaye anasikia mauamivu makali na pia hutumika kama dawa ya usingizi.

Alidai kuwa, hawezi kuthibitisha mshitakiwa alitumia dawa hizo kwa ajili ya nini kwa, isipokuwa kitaalamu zinaweza kutumiwa na mgonjwa kutokana na ushauri wa daktari.

Manji anatetewa na Wakili Hudson Ndusyepo, kesi hiyo itatolewa uamuzi kesho iwapo mshitakiwa ana kesi ya kujibu au la.

No comments:

Post a Comment