Thursday, 3 September 2015

JK AAGIZA MIKUTANO YA KAMPENI ILINDWE



Na Mwandishi Wetu

RAIS Jakaya Kikwete, ameyaelekeza majeshi ya ulinzi na usalama nchini kulinda mikutano ya kampeni za uchaguzi mkuu na kulinda mchakato mzima wa uchaguzi huo ili kushamirisha zaidi demokrasia ya Tanzania.

Akizungumza na maofisa wa Jeshi la Ulinzi la Wananchiwa Tanzania (JWTZ), Jeshi la Polisi, Jeshi la Magereza, Idara ya Usalama wa Taifa na Idara ya Uhamiaji usiku wa juzi, Rais Kikwete alisema majeshi ya ulinzi na usalama ya Tanzania yana wajibu wa pekee wa kulinda ustawi wa demokrasia ya Tanzania katika kipindi cha sasa cha kampeni na uchaguzi mkuu.

Rais Kikwete na Amiri Jeshi Mkuu alikuwa anazunguza na maofisa hao katika  halfa ya kumuaga kama Rais na Amiri  Jeshi Mkuu, iliyoandaliwa na majeshi hayo kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, mjini Dar es Salaam.

“Sasa tuko katika kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu na ni kipindi chenye changamoto nyingi, iwe ni wakati wa kampeni zenyewe, wakati wa upigaji kura na baada ya kupiga kura. Lindeni mikutano ya kampeni ya vyama vyote ili mikutano hiyo ifanyike kwa salama na amani,” alisema Rais Kikwete.

Aliongeza: “Lindeni usalama wa kati na siku ya kupigakura, lindeni usalama baada ya kumalizika uchaguzi mkuu kwa nia ya kuhakikisha kuwa demokrasia yetu changa inazidi kukua na kushamiri na nchi yetu inabakia tulivu na yenye amani.”

Halfa hiyo ya kumuaga Rais Kikwete ilikuwa tukio la mwisho katika siku ambayo majeshi ya Tanzania yalimuaga Amiri Jeshi Mkuu wao kwa shughuli mbalimbali.

Mapema asubuhi, majeshi yalimwandalia Rais Kikwete gwaride rasmi la kumuaga katikaUwanja wa Uhuru mjini Dar es Salaam.

Baadaye, Rais Kikwete alitunuku nishani za Utumishi Uliotukuka Tanzania, Utumishi Mrefu Tanzania na Utumishi MrefunaTabiaNjema, katika sherehe iliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam.

Nishani hizo walitunukiwa maofisa walio bado kwenye utumishi wa majeshi ya ulinzi na usalama nchini.

No comments:

Post a Comment