Thursday, 10 December 2015

BREAKING NYUZZZZ...: RAIS MAGUFULI ATANGAZA BARAZA JIPYA LA MAWAZIRI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitangaza baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es salaam leo Desemba 10, 2015.Kulia kwake ni Makamu wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan na kushoto ni Waziri Mkuu, Mhe. Majaliwa Kassim Majaliwa.


RAIS Jon Magufuli ametangaza baraza lake la mawaziri leo, alipokutana na waandishi wa habari, Ikulu mjini Dar es Salaam.

Rais Magufuli ametangaza baraza hilo mbele ya Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu Majaliwa Kassim na Katibu Mkuu Kiongozi, Ombeni Sefue.

Rais Magufuli amesema baraza lake litakuwa na mawaziri 19, ambapo baadhi ya wizara zitakuwa na mawaziri bila ya manaibu mawaziri. Amesema lengo la kupunguza ukubwa wa baraza la mawaziri ni kubana matumizi.

Aidha, amesema zilitengwa shilingi bilioni mbili ili mawaziri watakapoteuliwa wapelekwe semina elekezi, lakini semina hiyo sasa haitakuwepo, badala yake mawaziri wataanza kazi moja kwa moja.

Amesema fedha zilizopangwa kutumika kwenye semina hiyo, zitatumika sehemu nyingine kama vile kwenye elimu bure na kununua madawati.

BARAZA LA MAWAZIRI
 
Wizara ya Ofisi ya Rais,Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora.

Mawaziri - George Simbachakene  na Angella Kairuki

Naibu Waziri - Sumeilam Jafo. Naibu.

Wizara ya Ofisi ya Makamu wa Raisi, Muungano na Mazingira

Waziri - January Makamba

Naibu Waziri – Luhaga Jerrson Mpina


Ofisi ya Waziri Mkuu: Sera, Bunge, Kazi Vijana, Ajira na Walemavu

Waziri - Jenista Muhagama

MaNaibu – Dkt. Possy Abdallah na Anthony Mavunde.


Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi

Waziri - Mwigulu Nchemba

Naibu Waziri - William Ole Nasha


Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano.

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Edwin Ambandusi Ngonyani


Wizara ya Fedha na Mipango

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri - Ashantu Kizachi
 
Wizara ya Nishati na Madini

Waziri - Prof. Mwigalumi Muhongo.

Naibu Waziri - Medalled Karemaligo.


Wizara ya Katiba na Sheria,

Waziri - Harrison Mwakyembe


Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afika Mashariki, Kikanda na Kimataifa.

Waziri - Dk. Augustino Mahiga

Naibu Waziri – Dkt. Susan Kolimba.


Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa

Waziri - Dk. Hussein Mwinyi


Wizara ya Mambo ya Ndani

Waziri
- Charles Kitwanga.


Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi.

Waziri - William Lukuvi

Naibu Waziri - Angelina Mabula


Wizara ya Maliasili na Utalii

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri– Inj. Ramol Makani


Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji.

Waziri Charles Mwijage.


Wizara ya Elimu,Sayansi Teknolojia na Ufundi.

Waziri Bado hajapatikana.

Naibu Waziri – Inj. Stella Manyanya


Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto


Waziri - Ummy Mwalim

Naibu Waziri –  Dkt. Hamis Kigwangala


Wizara ya Habari, Utamaduni, Wasanii na Michezo

Waziri - Nape Nnauye

Naibu Waziri - Anastasia Wambura.


Wizara ya Maji na Umwagiliaji
Waziri – Prof. Makame Mbarawa

Naibu  Waziri– Inj. Isack Kamwela

No comments:

Post a Comment